Kutokana na haya tunasema kuwa Qadar imegawanyika sampuli nne:

1- Makadirio ya milele. Hayo ni yale yaliyotajwa katika Hadiyth ya kalamu.

2- Makadirio ya umri. Hayo ni yale yaliyotajwa katika Hadiyth ya Ibn Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anh).

3- Makadirio ya mwaka. Hayo ni yale yaliyotajwa katika usiku wa Qadar na yanahusiana na yatayokuwepo mwakani.

4- Makadirio ya siku. Ni yale yote ambayo Malaika wanaandika kutoka kwa waja katika madaftari yao.

Sampuli zote tatu za mwisho zina chanzo chake katika ile sampuli ya kwanza. Imani ya muumini haitimii mpaka ayaamini yote hayo pasi na kuwa na mashaka yoyote. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema wakati Jibriyl alipokuja kwake:

“… na kuamini Qadar, kheri na shari yake.”[1]

[1] Muslim (8) kupitia kwa ´Umar bin al-Khattwaab (Radhiya Allaahu ´anh).

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Itmaam-ul-Minnah, uk. 94-95
  • Imechapishwa: 08/04/2019