Maalik alikuwa akikosoa maneno mengi na kufutu na akisema juu ya yule mwenye kuingia katika mambo hayo:

“Ambaye anaropoka ni kama ngamia mwitu.”

Alikuwa akichukia kujibu maswali mengi na akisema:

“Allaah (´Azza wa Jall) amesema:

وَيَسْأَلُونَكَ عَنِ الرُّوحِ ۖ قُلِ الرُّوحُ مِنْ أَمْرِ رَبِّي وَمَا أُوتِيتُم مِّنَ الْعِلْمِ إِلَّا قَلِيلًا

“Wanakuuliza kuhusu roho. Sema: “Roho ni katika amri ya Mola wangu.” na hamkupewa ujuzi isipokuwa kidogo tu.”[1]

Hakutoa (Ta´ala) juu ya jambo hilo jibu lolote.”

Wakati mmoja aliulizwa juu ya mtu ambaye ni mtambuzi wa Sunnah kujadiliwe juu yake, akasema:

“Hapana. Asimulie Sunnah. Akikubaliwa ni vyema vinginevyo anyamaze.”

Amesema tena:

“Elimu ya mivutano na mijadala inazima nuru ya elimu.”

Amesema vilevile:

“Elimu ya mivutano inaufanya moyo kuwa msusuwavu na inapelekea chuki.”

Alikuwa akijibu juu ya maswali yanayouliziwa sana:

“Sijui.”

Imaam Ahmad alikuwa akifanya vivo hivyo. Licha ya haya Salaf na maimamu, kama vile Maalik, ash-Shaafi´iy, Ahmad na Ishaaq, wamebainisha namna ambavo Fiqh na hukumu zinatakiwa kuchukuliwa na kufahamika kwa njia fupi na ya mukhtasari.

[1] 17:85

  • Mhusika: Imaam Zayn-ud-Diyn bin Rajab al-Hanbaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bayaan Fadhwl ´Ilm-is-Salaf ´alaa ´Ilm-il-Khalaf, uk. 59-60
  • Imechapishwa: 21/09/2021