Kushabibisha ni kumthibitishia Allaah anayeshabihiana Naye katika zile haki au sifa ambazo ni maalum Kwake. Huu ni ukafiri. Kwa sababu ni katika kumshirikisha Allaah. Aidha kumekusanya kutia upungufu katika haki ya Allaah kwa vile amemshabihisha na viumbe ambao ni wapungufu.

Kufananisha ni kumthibitishia Allaah anayefanana Naye katika zile haki na sifa ambazo ni maalum Kwake. Ni ukafiri. Kwa sababu ni katika na kumkadhibisha na kumshirikisha Allaah. Amesema (Ta´ala):

لَيْسَ كَمِثْلِهِ شَيْءٌ ۖ وَهُوَ السَّمِيعُ الْبَصِيرُ

”Hakuna chochote kinachofanana Naye – Naye ni Mwenye kusikia, Mwenye kuona.”[1]

Aidha kumekusanya kutia upungufu katika haki ya Allaah kwa vile amemshabihisha na viumbe ambao ni wapungufu.

Tofauti kati ya kushabibisha na kufananisha ni kwamba kufananisha kunapelekea kulinganisha katika kila njia tofauti na kushabihisha.

[1] 42:11

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ta´aliyq mukhtaswar ´alaa Lum´at-il-I´tiqaad, uk. 34
  • Imechapishwa: 13/10/2022