Swali: Ni ipi hukumu mfungaji kumeza mate?

Jibu: Hakuna neno kumeza mate. Sijui kama kuna tofauti yoyote juu ya hilo wanachuoni kutokana na ule uzito na ugumu wa kujiepusha na hilo.

Kuhusu makohozi[1] ni lazima kwa mtu kuyatema pale yanapofika kinywani. Haijuzu kwa mfungaji kuyameza kwa sababu kuna uwezekano wa kuyaepuka tofauti na mate.

[1] Tazama https://firqatunnajia.com/kumeza-makohozi-kunaharibu-swawm-ya-mtu/

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ashyaa´ laa tufsid-is-Swawm, uk. 13
  • Imechapishwa: 01/04/2021