Swali: Je, kutapika kunaharibu swawm?

Jibu: Mara nyingi mfungaji anafikwa na mambo ambayo hakuyakusudia kukiwemo madonda, kutokwa na damu puani, kutapika, maji au petroli kuingia kooni mwake pasi na kutaka kwake. Mambo yote haya hayaharibu funga. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Ambaye yatamshinda matapishi hakuna juu yake kulipa na ambaye atajitapisha basi alipe.”

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ashyaa´ laa tufsid-is-Swawm, uk. 12-13
  • Imechapishwa: 01/04/2021