Abu Ma´mar al-Qutwiy´iy amesema:

”Mwisho wa maneno ya Jahmiyyah ni kwamba hakuna juu ya mbingu mungu yeyote.”

Ameipokea Abu Haatim.

Bishr al-Haafiy amesema:

”Tunaamini kwamba Allaah amelingana juu ya ´Arshi Yake, kama Anavyotaka, na kwamba Yeye ni Mjuzi wa kila mahali.”

Ameipokea Ibn Battwah na wengineo.

Harb bin Ismaa´iyl amesema:

”Nilimuuliza Ishaaq bin Raahawayh: ”Unasemaje juu ya maneno Yake Allaah (Ta´ala):

مَا يَكُونُ مِن نَّجْوَىٰ ثَلَاثَةٍ إِلَّا هُوَ رَابِعُهُمْ

“Hauwi mnong’ono wa watatu isipokuwa Yeye ni wa nne wao.”[1]

Akajibu: ”Popote ulipo basi Yeye yukaribu zaidi nawe kuliko mshipa wa shingo na wakati huohuo Yeye ametengana mbali na viumbe Vyake.” Amemnukuu Ibn-ul-Mubaarak, ambaye amesema kuwa Yuko juu ya ´Arshi Yake na ametengana mbali na viumbe Wake, kisha akasema: ”Kilicho juu zaidi ya hayo na kilicho na nguvu zaidi ni maneno Yake (Ta´ala):

الرَّحْمَـٰنُ عَلَى الْعَرْشِ اسْتَوَىٰ

”Mwingi wa rehema amelingana juu ya ´Arshi.”[2]

Ameipokea al-Khalaal katika “as-Sunnah”.

Yuusuf bin Muusa, na si al-Qattwaan, ameeleza:

”Ilisemwa kuambiwa ´Abdillaah Ahmad bin Hanbal: “Allaah yuko juu ya mbingu ya saba juu ya ´Arshi Yake, mbali na viumbe Vyake, ilihali uwezo Wake na ujuzi Wake viko kila mahali?” Akajibu: ”Ndiyo.”

Ameipokea al-Khallaal katika ”as-Sunnah”.

Dhuun-Nuun al-Miswriy amesema:

”Nuru Yake imezing’arisha mbingu, uso Wake umeangaza giza, utukufu Wake umefichwa na macho na humnong´oneza juu ya ´Arshi Yake  ndimi za vifuani.”

Ameipokea Abush-Shaykh katika ”al-´Adhwamah”.

Ahmad bin Salamah amesimulia ya kwamba amemsikia Ishaaq bin Raahuuyah akisema:

”Nilikutanishwa na huyu mzushi – akimaanisha Ibraahiym bin Abiy Swaalih – kwenye kikao cha gavana ´Abdullaah bin Twaahir. Gavana akaniuliza kuhusiana na Hadiyth za Kushuka anbapo nikazisoma. Akasema Ibn Abiy Saalih: “Nimememkufuru Mola anayeshuka kutoka mbingu moja hadi mbingu nyingine.” Ndipo nikasema: “Nimemwamini Mola anayefanya atakacho.”

Ameipokea al-Bayhaqiy na wengineo.

[1] 58:7

[2] 20:5

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Ahmad bin ´Abdil-Haadiy al-Maqdisiy (afk. 744)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Kalaam ´alaa Mas-alat-il-Istiwaa’ ´alaal-´Arsh, uk. 63-65
  • Imechapishwa: 23/12/2025