Mtunzi (Rahimahu Allaah) amesema:
“Hakuna upotofu wowote kwa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah… “
Hakuna upotofu wowote kwa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah kwa yale waliyokuja nayo Mitume kwa sababu ndio Njia ilinyooka. Njia hiyo ni kumpwekesha Allaah, kumtii, kuamini majina na sifa Zake na kwamba Yeye hana anayeshabihiana Naye, hana anayelingana Naye na wala hana mshirika na mwenza (Subhaanahu wa Ta´ala). Hii ndio njia iliyonyooka. Njia ambayo Allaah amesema juu yake:
اهْدِنَا الصِّرَاطَ الْمُسْتَقِيمَ
“Tuongoze njia iliyonyooka.” (01:06)
Njia hiyo ni:
الَّذِينَ أَنْعَمَ اللَّـهُ عَلَيْهِم مِّنَ النَّبِيِّينَ وَالصِّدِّيقِينَ وَالشُّهَدَاءِ وَالصَّالِحِينَ
“Wale Allaah aliowaneemesha miongoni mwa Manabii na wakweli mno na mashuhadaa na waja wema.” (04:69)
Njia yao ni kumuamini Allaah na majina na sifa Zake na wakati huohuo mtu amtakase Allaah kufanana na viumbe Wake na badala yake amsifu kwa sifa kamilifu, kutii maamrisho Yake, kujiepisha makatazo Yake na kusimama katika mipaka Yake. Hii ndio njia iliyonyooka. Njia hiyo ni ile:

“Wale Allaah aliowaneemesha miongoni mwa Manabii na wakweli mno na Mashuhadaa na waja wema.”
Amekusanya kati ya upambanuzi katika kuthibitisha na ujumla katika ukanushaji pale aliposema:
قُلْ هُوَ اللَّـهُ أَحَدٌ اللَّـهُ الصَّمَدُ لَمْ يَلِدْ وَلَمْ يُولَدْ وَلَمْ يَكُن لَّهُ كُفُوًا أَحَدٌ
”Sema: “Yeye ni Allaah Mmoja pekee. Allaah ambaye ni Mwenye kukusudiwa. Hakuzaa na wala hakuzaliwa. Na wala hana yeyote anayefanana [wala kulingana] Naye.”(112:01-04)
Amesema kuwa Yeye ndiye Allaah, Mmoja pekee na ndiye Mwenye kukusudiwa katika mambo yote. Halafu akasema:
لَمْ يَلِدْ وَلَمْ يُولَدْ
”Hakuzaa na wala hakuzaliwa.”
Huu ni ufafanuzi maalum ambapo ndani yake amekanusha kuwa na mwana, kwa sababu jambo hilo linapelekea katika mapungufu. Kisha akasema (Ta´ala):
وَلَمْ يَكُن لَّهُ كُفُوًا أَحَدٌ
“… na wala hana yeyote anayefanana [wala kulingana] Naye.” (112:04)
Vivyo hivyo maneno Yake (Ta´ala):
هَلْ تَعْلَمُ لَهُ سَمِيًّا
“Je, unamjua [mwengine] mwenye jina kama Lake?” (19:65)
فَلَا تَجْعَلُوا لِلَّـهِ أَندَادًا وَأَنتُمْ تَعْلَمُونَ
“Basi msimfanyie Allaah waliolingana naye [washirika] na hali ya kuwa nyinyi mnajua [kuwa hana].” (02:22)
لَيْسَ كَمِثْلِهِ شَيْءٌ ۖ وَهُوَ السَّمِيعُ الْبَصِير
“Hakuna chochote kinachofanana Naye – Naye ni Mwenye kusikia, Mwenye kuona.” (42:11)
- Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh al-´Aqiydah al-Waasitwiyyah, uk. 23-24
- Imechapishwa: 17/10/2024
Mtunzi (Rahimahu Allaah) amesema:
“Hakuna upotofu wowote kwa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah… ”
Hakuna upotofu wowote kwa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah kwa yale waliyokuja nayo Mitume kwa sababu ndio Njia ilinyooka. Njia hiyo ni kumpwekesha Allaah, kumtii, kuamini majina na sifa Zake na kwamba Yeye hana anayeshabihiana Naye, hana anayelingana Naye na wala hana mshirika na mwenza (Subhaanahu wa Ta´ala). Hii ndio njia iliyonyooka. Njia ambayo Allaah amesema juu yake:
اهْدِنَا الصِّرَاطَ الْمُسْتَقِيمَ
“Tuongoze njia iliyonyooka.” (01:06)
Njia hiyo ni:
الَّذِينَ أَنْعَمَ اللَّـهُ عَلَيْهِم مِّنَ النَّبِيِّينَ وَالصِّدِّيقِينَ وَالشُّهَدَاءِ وَالصَّالِحِينَ
“Wale Allaah aliowaneemesha miongoni mwa Manabii na wakweli mno na mashuhadaa na waja wema.” (04:69)
Njia yao ni kumuamini Allaah na majina na sifa Zake na wakati huohuo mtu amtakase Allaah kufanana na viumbe Wake na badala yake amsifu kwa sifa kamilifu, kutii maamrisho Yake, kujiepisha makatazo Yake na kusimama katika mipaka Yake. Hii ndio njia iliyonyooka. Njia hiyo ni ile:
الَّذِينَ أَنْعَمَ اللَّـهُ عَلَيْهِم مِّنَ النَّبِيِّينَ وَالصِّدِّيقِينَ وَالشُّهَدَاءِ وَالصَّالِحِينَ
“Wale Allaah aliowaneemesha miongoni mwa Manabii na wakweli mno na Mashuhadaa na waja wema.”
Amekusanya kati ya upambanuzi katika kuthibitisha na ujumla katika ukanushaji pale aliposema:
قُلْ هُوَ اللَّـهُ أَحَدٌ اللَّـهُ الصَّمَدُ لَمْ يَلِدْ وَلَمْ يُولَدْ وَلَمْ يَكُن لَّهُ كُفُوًا أَحَدٌ
”Sema: “Yeye ni Allaah Mmoja pekee. Allaah ambaye ni Mwenye kukusudiwa. Hakuzaa na wala hakuzaliwa. Na wala hana yeyote anayefanana [wala kulingana] Naye.”(112:01-04)
Amesema kuwa Yeye ndiye Allaah, Mmoja pekee na ndiye Mwenye kukusudiwa katika mambo yote. Halafu akasema:
لَمْ يَلِدْ وَلَمْ يُولَدْ
”Hakuzaa na wala hakuzaliwa.”
Huu ni ufafanuzi maalum ambapo ndani yake amekanusha kuwa na mwana, kwa sababu jambo hilo linapelekea katika mapungufu. Kisha akasema (Ta´ala):
وَلَمْ يَكُن لَّهُ كُفُوًا أَحَدٌ
“… na wala hana yeyote anayefanana [wala kulingana] Naye.” (112:04)
Vivyo hivyo maneno Yake (Ta´ala):
هَلْ تَعْلَمُ لَهُ سَمِيًّا
“Je, unamjua [mwengine] mwenye jina kama Lake?” (19:65)
فَلَا تَجْعَلُوا لِلَّـهِ أَندَادًا وَأَنتُمْ تَعْلَمُونَ
“Basi msimfanyie Allaah waliolingana naye [washirika] na hali ya kuwa nyinyi mnajua [kuwa hana].” (02:22)
لَيْسَ كَمِثْلِهِ شَيْءٌ ۖ وَهُوَ السَّمِيعُ الْبَصِير
“Hakuna chochote kinachofanana Naye – Naye ni Mwenye kusikia, Mwenye kuona.” (42:11)
Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Sharh al-´Aqiydah al-Waasitwiyyah, uk. 23-24
Imechapishwa: 17/10/2024
https://firqatunnajia.com/15-hii-ndio-njia-wanayofuata-ahl-us-sunnah-al-jamaaah/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)