Inapendekeza kuomba du´aa anayotaka wakati wa kukata funga yake. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakika mfungaji anayo du´aa isiyorudishwa nyuma wakati wa kufutari.”[1]

Miongoni mwa du´aa zilizopolewa ni yeye aombe kwa kusema:

اللَّهُمَّ لَكَ صُمْتُ وَعَلَى رِزْقِكَ أَفْطَرْتُ

“Ee Allaah! Nimefunga kwa ajili yako na nimefutari kwa riziki yako.”[2]

 Alikuwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wakati anapokata funga husema:

ذَهَبَ الظَّمَأُ وَابْتَلَّتِ الْعُرُوقُ وَثَبَتَ الْأَجْرُ إِنْ شَاءَ اللَّهُ

“Kiu kimeondoka, mishipa imerowana na ujira umepatikana – Allaah akitaka.”[3]

Namna hii muislamu anatakiwa kujifunza hukumu za funga, ukataji swawm, wakati na sifa yake ili aweze atekeleze funga yake kwa njia iliyowekwa katika Shari´ah inayoafikiana na Sunnah ya Mtume (Swalla Allahau ´alayhi wa sallam). Ili pia funga yake iweze kuwa sahihi na yenye kukubaliwa mbele ya Allaah. Hilo ni miongoni mwa mambo muhimu. Amesema (Ta´ala):

لَّقَدْ كَانَ لَكُمْ فِي رَسُولِ اللَّـهِ أُسْوَةٌ حَسَنَةٌ لِّمَن كَانَ يَرْجُو اللَّـهَ وَالْيَوْمَ الْآخِرَ وَذَكَرَ اللَّـهَ كَثِيرًا

“Hakika mna kigezo chema kwa Mtume wa Allaah kwa yule mwenye kumtaraji Allaah na siku ya Mwisho na akamtaja Allaah kwa wingi.”[4]

[1] Ibn Maajah (1753).

[2] Abu Daawuud (2358).

[3] Abu Daawuud (2357).

[4] 33:21

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Mulakhasw al-Fiqh (01/381)
  • Imechapishwa: 03/04/2021