Hapa kuna jambo ambalo ni lazima kulizindua. Baadhi ya watu wanaweza kukaa katika meza ya futari na wakala chakula cha jioni na wakaacha kuswali maghrib pamoja na mkusanyiko msikitini. Kwa kufanya hivo wanakuwa wamefanya kosa kubwa ambalo ni kuchelewesha swalah ya mkusanyiko msikitini na akajikosesha mwenyewe thawabu nyingi na akajiweka katika khatari ya adhabu. Kilichowekwa katika Shari´ah kwa mfungaji ni yeye kufuturu kwanza kisha aende kuswali. Baada ya hapo ndio ale chakula cha jioni.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Mulakhasw al-Fiqh (01/381)
  • Imechapishwa: 03/04/2021