Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:
10- Hafanani na viumbe/watu.
MAELEZO
Hii ni kama ile ibara iliotangulia. Hakuna kitu mfano Wake. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) ametakasika kufanana na viumbe:
لَيْسَ كَمِثْلِهِ شَيْءٌ ۖوَهُوَ السَّمِيعُ الْبَصِيرُ
“Hakuna chochote kinachofanana Naye – Naye ni Mwenye kusikia, Mwenye kuona.”[1]
وَلَمْ يَكُن لَّهُ كُفُوًا أَحَدٌ
”Wala hakuna yeyote anayefanana na kulingana Naye.”[2]
Yeye (Subhaanah) hafanani na viumbe Wake. Hata kama ana majina na sifa ambazo zinashirikiana na majina na sifa za viumbe katika utamkaji na maana, lakini kuna tofauti katika uhakika na namna. Kwa njia hiyo hakuna ufanano.
[1] 42:11
[2] 112:04
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 37
- Imechapishwa: 12/09/2019
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)