al-Halabiy amesema:
“Kadhalika inahusiana na Tabdiy´ kwa Haafidhw Ibn Hajar na Haafidhw an-Nawawiy. Hata kama Shaykh Rabiy´ hawafanyii Tabdiy´ya wazi wazi lakini hata hivyo haonelei tofauti kubwa kati ya kwamba walikuwa ni Ashaa´irah waliotumbukia kwenye Bid´ah na kwamba ni watu wa Bid´ah. Inahusiana tu na ibara za kujiheshimu. Amesema pindi alipoulizwa juu ya tofauti kati ya Haddaadiyyah na Salafiyyah:
“Moja katika sifa zao ni kwamba hawarehemu. Ukimtakia rahmah Ibn Hajar, ash-Shawkaaniy na an-Nawawiy wanasema: “Mtu wa Bid´ah!” Ukisema “Haafidhw wao wanasema “Mtu wa Bid´ah!” Ukiwaambia kuwa walitumbukia kwenye makosa ya Ashaa´irah wanasema: “Ni lazima useme kuwa ni watu wa Bid´ah. La sivyo wewe ndio mtu wa Bid´ah!” Tukiwaambia kuwa mtu ambaye ni Ash´ariy hiyo ina maana kwamba mtu huyu ana Bid´ah. Mtu anataka kuzungumza kwa heshima. Sio lazima useme kuwa ni mtu wa Bid´ah. Wakati al-Bukhaariy anapowapitia wapokezi kama Jaabir al-Ju´fiy na wengine hasemi kuwa ni mtu wa Bid´ah ijapokuwa anajua kuwa alikuwa ni Raafidhwiy. Hasemi kuwa ni mtu wa Bid´ah kwa kuwa sio jambo la lazima. Bainisha upotevu wake kwa ajili ya kuwatakia watu mema, lakini huhitajii kusema kuwa ni mtu wa Bid´ah. Hawakukubali. Kuna mtu alinipigia simu kutoka Abhaa na kuniuliza maoni yangu juu ya Ibn Hajar. Nikawaambia kuwa alikuwa na makosa ya Ashaa´irah. Akanambia kuwa mimi ni mpotevu na kwamba ni lazima niseme kuwa ni mtu wa Bid´ah.”
Shaykh Rabiy´ anawakemea Haddaadiyyah kwa kumlazimisha kumfanyia Tabdiy´ mtu ambaye alitumbukia kwenye makosa ya Ashaa´irah bali kwenye Bid´ah za Raafidhwah ilihali ya kwamba yeye mwenyewe analazimisha kuwafanyia Tabdiy´ Salafiyyuun. Ni nani aliye karibu na Haddaadiyyah? Ni yeye au wale anaowakemea?”[1]
Ibn Hajar na an-Nawawiy wote wawili walikuwa na makosa ya Ashaa´irah. Ndio maana Imaam Ibn Baaz alikemea mengi katika makumi ya makosa ya ki-Ash´ariy ya Ibn Hajar na akamuomba ash-Shibl kukamilisha radd yake kwa Ibn Hajar, jambo ambalo alilifanya. Mashhuur Hasan aliraddi makosa ya ki-Ash´ariy ya an-Nawawiy kwenye ufafanuzi wake wa “as-Swahiyh” ya Muslim. Hata na mimi niliraddi makosa ya ki-Ash´ariy ya an-Nawawiy.
Ama kuhusiana na Haddaadiyyah, wao wanamfanyia Tabdiy´ Ibn Hajar na an-Nawawiy na wale wasiowafanyia Tabdiy´. Wanawalenga Salafiyyuun. Wakaunguza “Fath-ul-Baariy” ambapo wanachuoni Salafiyyuun kama Ibn Baaz, al-Albaaniy, Ibn ´Uthaymiyn, al-Fawzaan, al-Luhaydaan na wengine wakakemea kitendo hicho. Lau ungelikuwa unawaheshimu wanachuoni hawa ambao wana maoni mamoja na mimi basi usingelinitukana. Salafiyyuun wanachuoni na wanafunzi wanajua ni makosa yepi ya ki-Ash´ariy alionayo an-Nawawiy na Ibn Hajar. Lakini pamoja na hivyo makosa yao hayazingatiwi ni kama makosa ya wanafalsafa na Ashaa´irah waliopindukia – kama makosa ya ar-Raaziy. Wanaona kuna tofauti kubwa kati ya hao wawili na wanafalsafa wa Ashaa´irah kwa vile wao wametumia maisha yao yote kuitumikia Sunnah ya Mtume katika nyanja nyingi. Wameifafanua, kuandika wasifu wa wapokezi wake, kubainisha hali za wapokezi wake kwa kuwakosoa na kuwasifu, wakatunga kuhusu elimu ya Hadiyth pamoja na kuwapenda kwao Ahl-ul-Hadiyth. an-Nawawiy ameandika ikiwa ni pamoja na:
1 – Sharh Swahiyh Muslim
2 – Riyaadh-us-Swaalihiyn
3 – al-Adhkaar
4 – Tahdhiyb-ul-Asmaa’ wal-Lughaat
5 – al-Irshaad
6 – at-Taqriyb
7 – al-Majmuu´
Ni mwenye kupita katika mfumo wa Ahl-ul-Hadiyth inapokuja katika kutumia hoja katika masuala ya ki-Fiqh. Hakuandika kitabu chochote juu ya ´Aqiydah ya Ashaa´irah na kuitetea.
Haafidhw Ibn Hajar ana vitabu vingi ambapo ameitumikia Sunnah ya Mtume ikiwa ni pamoja na:
1 – Ittihaaf-ul-Maharah bi Atwraaf-il-´Asharah
2 – al-Iswaabah fiy Tamyiyz-is-Swahaabah
3 – Inbaa’-ul-Ghamar
4 – Buluugh-ul-Maraam
5 – Tabswiyr-ul-Muntabih
6 – Tajriyd-ul-Asaaniyd
7 – Ta´jiyl-ul-Manfa´ah
8 – Taghliyq-ut-Ta´liyq
9 – Taqriyb-ut-Tahdhiyb
10 – al-Talkhiysw al-Habiyr…
Wote wawili wanaenda kinyume na wanafalsafa wa Ashaa´irah katika mambo ya ´Aqiydah ya msingi. Tofauti hii kubwa kati yao na kati ya wanafalsafa wa Ashaa´irah inawafanya Salafiyyuun Saudi Arabia kuwakemea wale wenye kuwafanyia Tabdiy´ – kama wafanyavyo Haddaadiyyah. ´Allaamah al-Albaaniy aliwakemea vibaya sana pindi aliposema:
“Sio kila mwenye kutumbukia katika Bid´ah anakuwa ni mtu wa Bid´ah.”
Yeye mwenyewe anakiri kuwa Ibn Hajar na an-Nawawiy wote wawili walitumbukia katika Bid´ah lakini hata hivyo hawafanyii Tabdiy´. Yeye pia ni mwenye kujigonga? Wale wenye kukemea makosa yao ya ki-Ash´ariy bila ya kuwafanyia Tabdiy´ wanakuwa pia watu wa Bid´ah? Ni kwa nini hukuwatuhumu pia na wao kuwa ni wenye kujigonga? Je, huku si ndo kule kujigonga kwa matamanio ambako kumeshabihiana na hukumu za mayahudi pindi wanapowasamehe wale waliokuwa na nguvu na kuwaadhibu walio wadhaifu?
Halafu tazama jinsi al-Halabiy anavojua wanayosema Haddaadiyyah pasina kuwakemea. Bali anafikia mpaka kuhoji kwa madhambi yao dhidi yangu. Je, huku si katika kupakana mafuta na wenye kudhulumu na kuwashambulia wasiokuwa na hatia?
Niko macho bara bara kwa Haddaadiyyah kuliko walivo wengine. Najua matusi yao kwa Ibn Hajar na an-Nawawiy wanawakusudia maimamu wa Da´wah na khaswa Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah, Imaam Ibn-ul-Qayyim, Imaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab na kizazi na wanafunzi zake. Wakati Shaykh wa Haddaadiyyah alipomtukana Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah, Ibn-ul-Qayyim na Ibn Abiyl-´Izz mimi ndiye ambaye niliyemraddi al-Haddaad na si al-Halabiy wala pote lake halikufanya lolote.
Wakati al-Haddaad alipomtukana ´Allaamah al-Albaaniy na kuandika kitabu dhidi yake kilicho na maelfu ya kurasa al-Halabiy hakumraddi, ambaye amejificha nyuma ya al-Albaaniy.
Pengine al-Halabiy anafurahishwa kwa Salafiyyuun na maimamu kutukanywa kama jinsi anavyofurahishwa na watu wenye kuwachukia Salafiyyuun na wanachuoni wao zaidi ya Haddaadiyyah kama Abul-Hasan al-Ma´ribiy, al-Maghraawiy na ´Ar´uur. Watu hawa wanawapiga vita Salafiyyuun kiunyama. Waliwaangusha wanachuoni pindi walipowanasihi na kuwaomba warudishe misingi na upotevu wao yenye kwenda kinyume na mfumo wa Salaf. Hawakufanya hivo. Badala yake wakaendelea na ukandamizaji huu na kuwatetea Ahl-ul-Bid´ah walio na imani ya Wahdat-ul-Wujuud, Huluul, umoja wa dini na uhuru wa dini. Si al-Halabiy wala pote lake hawakukemea kitu katika hayo. Bali wamefikia mpaka kuwatetea na kutetea batili yao. Wanawaonelea kuwa ni Salafiyyuun na wale wenye kuraddi upotevu wao mkubwa ya kwamba ni wapetukaji mipaka. Bali uhakika wa mambo wao ndio wapetukaji mipaka.
Isitoshe Ibn Hajar na an-Nawawiy wamefanya vijimambo na kuvieneza ili kuwafarikanisha Salafiyyuun ulimwenguni kama jinsi pote la al-Halabiy lilivyofanya? Ni ipi hukumu ya wale wenye kuwalinda na kuwanusuru na kushirikiana nao katika kueneza fitina?
Mimi naitakidi ya kwamba mtu ambaye yuko bega kwa bega na watu wenye kulingania katika umoja wa dini, udugu wa dini na uhuru wa dini, kutetea upotevu huu, kusifu gazeti lililo na upotevu huu na kuwatetea wale wenye kulinusuru na kuwaita kuwa ni “wanachuoni waaminifu” ni mbaya zaidi kuliko Haddaadiyyah na bali ni mbaya zaidi kuliko hata Mu´tazilah na Khawaarij.
Radd makosa haya kwa maazimio na kiukweli na hakuna atayekuomba uwafanyie Tabdiy´. Hebu thubutu! Ni vipi mtu atatarajia uadilifu kutoka kwa mtu mwenye kufanya dhuluma ambaye ananusuru na kutetea wapotevu?
[1] Uk. 04-05
- Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: http://rabee.net/ar/articles.php?cat=8&id=236
- Imechapishwa: 08/01/2017

Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: http://rabee.net/ar/articles.php?cat=8&id=236
Imechapishwa: 08/01/2017
https://firqatunnajia.com/15-al-halabiy-anamtuhumu-rabiy-al-madkhaliy-kumfanyia-tabdiy-an-nawawiy-na-ibn-hajar/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)