Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:
121 – Kisha atawatoa humo kwa rehema Zake na kwa uombezi wa waja Wake watifiu watakaowaombea. Kisha atawaagiza katika Pepo Yake.
MAELEZO
Haya yamesihi kwa maelezo kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Watenda madhambi wapwekeshaji watatoka Motoni, ima kwa fadhilah za Allaah (Ta´ala) au kwa uombezi wa waombezi baada ya idhini ya Allaah. Uombezi ni haki, lakini utakuwa baada ya idhini ya Allaah. Jengine ni kwamba ni lazima yule anayeombewa awe miongoni mwa wale watu waliokuwa wakimwabudu Allaah pekee. Si makafiri, washirikina wala wanafiki hawana haki ya uombezi.
Baada ya kutolewa nje ya Moto, watatumwa Peponi. Abu Sa´iyd al-Khudriy amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Wakati watu wa Peponi watakapoingia Peponi na watu wa Motoni watakapoingia Motoni, Allaah atasema: “Mtoeni humo yule ambaye moyoni mwake mna imani sawa na mbegu ya haradali.” Watatolewa humo baada ya kuchomeka na kuwa majivu na watachovya kwenye mto wa uhai.”[1]
Baada ya hapo ndio wataingia Peponi.
[1]al-Bukhaariy (6560) na Muslim (184).
- Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 157-158
- Imechapishwa: 25/11/2024
Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:
121 – Kisha atawatoa humo kwa rehema Zake na kwa uombezi wa waja Wake watifiu watakaowaombea. Kisha atawaagiza katika Pepo Yake.
MAELEZO
Haya yamesihi kwa maelezo kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Watenda madhambi wapwekeshaji watatoka Motoni, ima kwa fadhilah za Allaah (Ta´ala) au kwa uombezi wa waombezi baada ya idhini ya Allaah. Uombezi ni haki, lakini utakuwa baada ya idhini ya Allaah. Jengine ni kwamba ni lazima yule anayeombewa awe miongoni mwa wale watu waliokuwa wakimwabudu Allaah pekee. Si makafiri, washirikina wala wanafiki hawana haki ya uombezi.
Baada ya kutolewa nje ya Moto, watatumwa Peponi. Abu Sa´iyd al-Khudriy amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Wakati watu wa Peponi watakapoingia Peponi na watu wa Motoni watakapoingia Motoni, Allaah atasema: “Mtoeni humo yule ambaye moyoni mwake mna imani sawa na mbegu ya haradali.” Watatolewa humo baada ya kuchomeka na kuwa majivu na watachovya kwenye mto wa uhai.”[1]
Baada ya hapo ndio wataingia Peponi.
[1]al-Bukhaariy (6560) na Muslim (184).
Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 157-158
Imechapishwa: 25/11/2024
https://firqatunnajia.com/148-watatolewa-motoni-na-kuingizwa-peponi/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)