Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah amesema:
Wanaona kuwa maelezo ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kumuhusu Allaah na siku ya Mwisho si jengine isipokuwa tu ni dhana tu na mawazo yenye kuzuliwa. Malengo ya ujumbe ni ili wengi waweze kunufaika, na si kwamba yanabainisha haki, kuwaongoza viumbe wala kuweka wazi uhakika wa mambo. Kundi hili limegawanyika makundi mawili:
Kundi moja linasema kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakujua uhakika wa mambo yalivyo na kwamba wako wanafalsafa wa kimungu na pia wale mawalii wanaowadai ambao wameyajua. Kwa mujibu wao wanadai kuwa kuna wanafalsafa na mawalii ambao ni wajuzi zaidi juu ya Allaah na Qiyaamah kuliko Mitume. Maneno haya yanatoka kwa wakanamungu waliochupa mipaka katika wanafalsafa na Baatwiniyyah wa Shiy´ah na wa Suufiyyah.
MAELEZO
Wale watu wanaofuata mawazo wanadai kuwa hiki alichokisema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) si kweli na kwamba alisema mambo ya kufikirisha tu kwa ajili ya maslahi ya watu. Kwa hiyo ni uongo kwa ajili ya maslahi. Wakagawanyika makundi mawili:
1 – Wanaosema kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anajua ukweli lakini hakuwabainishia watu. Maana yake ni kuwapotosha watu.
2 – Wanaosema kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hajui ukweli naa ndio maana akasema kinyume chake. Huku ni kumfanya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuwa mjinga.
Wanafalsafa wamegawanyika sampuli mbili; wanafalsafa wanaokiri kuwepo kwa Allaah na wanafalsafa makafiri wasiokubali kuwepo kwa Mola. Watu hawa wanaona kuwa wanafalsafa ni mjuzi zaidi kuliko Mtume, na kwa Suufiyyah waliopotoka wanaona kuwa walii ana daraja ya juu zaidi kuliko Mtume. Kwa ajili hiyo wakasema:
Nafasi ya unabii iko katika sehemu ya kati
juu ya Mtume lakini chini ya walii[1]
Baatwiniyyah ni wale Shiy´ah waliopinduka mipaka, wakiwemo Ismaa´iyliyyah, Faatwimiyyah na Qaraamitwah. Miongoni mwao yapo makundi yanayodai kuwa Maandiko yana maana ya nje na maana ya ndani. Maana ya nje inatambulika kwa watu wa kawaida. Lakini maana ya ndani inatambulika tu na wale watu wao maalum. Miongoni mwa Baatwiniyyah wa Suufiyyah ni Ibn ´Arabiy, Ibn-ul-Faaridhw, Ibn Sab´iyn na al-Hallaaj.
[1] Tazama ”al-Futuuhaat al-Makkiyyah” (2/252) ya Ibn ´Arabiy.
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaa al-Hamawiyyah, uk. 240-241
- Imechapishwa: 20/07/2026

Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaa al-Hamawiyyah, uk. 240-241
Imechapishwa: 20/07/2026
https://firqatunnajia.com/147-wanaona-kuwa-wanafalsafa-na-mawalii-ni-bora-kuliko-mitume/