Mwanzoni Suufiyyah hawakuwa wamepotoka. Walikuwa ni watu wa ´ibaadah lakini wakijitaabisha nafsi zao, kama al-Junayd, Bishr al-Haafiy, Ibraahiym bin Ad-ham na al-Fudhwayl bin ´Iyaadhw. Hawa walikuwa watu wa ´ibaadah, wanazuoni na wenye kushikamana na ´Aqiydah sahihi. Lakini baadaye Taswawwuf ilibadilika ambapo zikapenya ndani yake Bid´ah na ikaingia Taswawwuf ya wanafalsafa kutoka kwa wahindi na wengineo. Pia ukaingia ushirikina wa makaburini, mpaka ukafikia itikadi ya kuona kuwa kila kitu ni Allaah na Allaah ni kila kitu (وحدة الوجود), kama ilivyo ´Aqiydah ya Ibn ´Arabiy, Ibn Sab´iyn na wale Suufiyyah wengine waliochupa mipaka.
Hivi ndivyo inavyokuwa kutoka nje ya Qur-aan na Sunnah, hata kama mwanzo wake ulikuwa kwa kusudio zuri na mapenzi ya kupenda kheri. Hatimaye huwapotosha wenyewe. Ama wale walioshikamana na Qur-aan na Sunnah, hawakufikia ukafiri na uzandiki. Hili linaonesha wajibu wa kushikamana na Qur-aan na Sunnah katika ´ibaadah na katika mambo mengine yote. Kheri yote imo ndani ya Qur-aan na Sunnah. Anas (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:
”Kundi la watu watatu lilikuja katika nyumba za wake wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wakiuliza kuhusu ´ibaadah ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Walipoambiwa, ni kama kwamba walizidogesha. Wakasema: “Sisi tuko wapi ukilinganisha na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hali ya kuwa amesamehewa yaliyotangulia katika madhambi yake na yatakayokuja baadaye?” Mmoja wao akasema: “Ama mimi, nitaswali usiku daima.” Mwingine akasema: “Mimi nitafunga mwaka mzima wala sitafungua.” Mwingine akasema: “Mimi nitajitenga na wanawake wala sitaoa kabisa.” Akaja Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kusema: “Je, nyinyi ndio mliosema hivi na hivi? Ama naapa kwa Allaah, hakika mimi ndiye mwenye kumkhofu Allaah na mwenye kumcha zaidi kuwashinda nyinyi. Lakini mimi mara nafunga na mara ninafungua, mara naswali na mara nalala na ninaoa wanawake. Hivyo basi atakayeiacha Sunnah yangu si katika mimi.”[1]
Kwa hiyo wastani, kunyooka na kushikamana na Qur-aan na Sunnah ndio kheri duniani na Aakhirah. Hakuna anayejitenga na Qur-aan na Sunnah isipokuwa huishia katika upotovu, hata kama mwanzo wa jambo lake alikuwa anataka kheri na nia yake ni nzuri. Lakini jambo huendelea kukua na shaytwaan hasimami katika mipaka; humvuta mtu hatua kwa hatua. Hakuna anayeweza kushindwa na shaytwaan isipokuwa yule anayesshikamana na Qur-aan na Sunnah.
Anayejifanya kuwa ni mwenye uelewa ni yule ambaye uelea wake haujakamilika ambapo anaidhuru nafsi yake mwenyewe na huwadhuru watu anapotoa fatwa bila elimu.
[1] al-Bukhaariy (5063) na Muslim (1401).
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaa al-Hamawiyyah, uk. 238-239
- Imechapishwa: 20/07/2026

Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaa al-Hamawiyyah, uk. 238-239
Imechapishwa: 20/07/2026
https://firqatunnajia.com/146-mwanzo-na-mwisho-wa-suufiyyah-mazingatio-kwa-wengine-wote/