Suufiyyah asili yake ni mtu anayezidisha sana katika kuipa nyongo dunia na ´ibaadah. Wametofautiana kuhusu sababu ya kuitwa kwao jina hilo. Baadhi yao wanasema Taswawwuf imetokana na sufu, kwa sababu Suufiyyah walikuwa wakivaa sufu na kujibana katika maisha. Hivyo wakaitwa Suufiyyah, kwa sababu alama yao ilikuwa kuvaa sufu kutokana na kuipa kisogo dunia. Maoni haya ndio yaliyo karibu zaidi na usawa.
Wengine wanasema waliitwa Suufiyyah kwa kuhusishwa na “Ahl-us-Suffah” waliokuwepo zama za Mtume Suufiyyah. Nao ni wale waliokuja Madiynah kutafuta elimu huku hawana jamaa wala mali humo. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akawaweka katika sehemu ya msikiti na akawalisha kutokana na swadaqah na yale ambayo Allaah amemrahisishia. Maoni haya si sahihi, kwa sababu kuna tofauti kati ya hawa na wale.
Wengine wanasema waliitwa Suufiyyah kutokana na “usafi” (الصفاء), kwa sababu nyoyo zao ni safi. Hili pia ni makosa.
Maoni sahihi ni yale ya kwanza. Waliitwa Suufiyyah kwa sababu walikuwa wakijibana, wakidhihirisha na ´ibaadah na kuipa nyongo dunia na wakivaa sufu.
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaa al-Hamawiyyah, uk. 238
- Imechapishwa: 20/07/2026
Suufiyyah asili yake ni mtu anayezidisha sana katika kuipa nyongo dunia na ´ibaadah. Wametofautiana kuhusu sababu ya kuitwa kwao jina hilo. Baadhi yao wanasema Taswawwuf imetokana na sufu, kwa sababu Suufiyyah walikuwa wakivaa sufu na kujibana katika maisha. Hivyo wakaitwa Suufiyyah, kwa sababu alama yao ilikuwa kuvaa sufu kutokana na kuipa kisogo dunia. Maoni haya ndio yaliyo karibu zaidi na usawa.
Wengine wanasema waliitwa Suufiyyah kwa kuhusishwa na “Ahl-us-Suffah” waliokuwepo zama za Mtume Suufiyyah. Nao ni wale waliokuja Madiynah kutafuta elimu huku hawana jamaa wala mali humo. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akawaweka katika sehemu ya msikiti na akawalisha kutokana na swadaqah na yale ambayo Allaah amemrahisishia. Maoni haya si sahihi, kwa sababu kuna tofauti kati ya hawa na wale.
Wengine wanasema waliitwa Suufiyyah kutokana na “usafi” (الصفاء), kwa sababu nyoyo zao ni safi. Hili pia ni makosa.
Maoni sahihi ni yale ya kwanza. Waliitwa Suufiyyah kwa sababu walikuwa wakijibana, wakidhihirisha na ´ibaadah na kuipa nyongo dunia na wakivaa sufu.
Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaa al-Hamawiyyah, uk. 238
Imechapishwa: 20/07/2026
https://firqatunnajia.com/145-chimbuko-la-neno-suufiyyah/