129 – Inajuzu kuchimbua makaburi ya makafiri, kwa sababu hayana heshima kama inavyojulisha na maana ya Hadiyth iliyotangulia. Vilevile hili linathibishwa na Hadiyth ya Anas bin Maalik (Radhiya Allaahu ´anh) ambaye ameeleza:
”Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alifika Madiynah ambapo akatua upande wa juu wa mji katika kabila linaloitwa ”Banuu ´Amr bin ´Awf”. Akakaa kwao kwa muda wa nyusiku kumi na minne, kisha akatuma ujumbe kwa Banuu an-Najjaar, wakaja wakiwa wamevaa panga zao. Ni kama ninamuona Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akiwa juu ya mnyama wake na Abu Bakr akiwa ameketi nyuma yake na kundi la Banuu an-Najjaar likiwa linamzunguka, mpaka alipofika katika uwanja wa Abu Ayyuub. Alikuwa akipenda kuswali pale ambapo swalah inamkuta na alikuwa akiswali katika malisho ya kondoo. Akaamuru kujengwa kwa msikiti. Akatuma ujumbe kwa kundi la Banuu an-Najjaar ambapo akasema: ”Enyi Banuu an-Najjaar, niuzieni ukuta wenu huu.” Wakasema: ”Hapana, tunaapa kwa Allaah kwamba hatutaki malipo yake isipokuwa kwa Allaah.” Akasema: ”Katika eneo hilo palikuwa na makaburi ya washirikina na eneo lililoharibika. Ndipo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akaamuru makaburi ya washirikina yachimbuliwe, kisha maeneo yaliyoharibika yasawazishwe na mitende ikatwe. Wakaipanga mitende upande wa Qiblah wa msikiti na akafanya mihimili yake iwe mawe. Wakaanza kubeba mawe huku wakitumbuiza kwa beti na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa pamoja nao naye alikuwa akisema [huku akibeba matofali]:
Hili ni mzigo wa Khaybar si kama mizigo mingine,
Hili linampendeza zaidi Mola wetu na ni safi zaidi
Ee Allaah, hakuna kheri isipokuwa kheri ya Aakhirah,
Basi wasamehe Answaar na Muhaajiruun.
Imekuaj katika riwaya nyingine kutoka kwa ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa):
”Ee Allaah! Hakika malipo ni malipo ya Aakhirah. Basi warehemu Answaar na Muhaajiruun.”
Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim na wengine kutoka kwa Anas ambaye muundo ni wake, al-Bukhaariy pia ameipokea kutoka kwa ´Aaishah. Kilicho ndani ya mabano ni katika mapokezi yake. Hadiyth hizi mbili nimezitaja katika “ath-Thamar al-Mustatwaab”.
Haafidhw amesema katika “al-Fath”:
”Katika Hadiyth kuna dalili ya uhalali wa kutumia kaburi lililomulikwa kwa njia ya zawadi au mauzo. Aidha inajuzu kuchimbua makaburi yaliyochakaa ikiwa si ya kuheshimiwa. Vilevile inajuzu kuswali katika sehemu ambazo zamani zilikuwa makaburi ya washirikina baada ya kuchimbuliwa na kuondolewa yaliyomo. Pia inajuzu kujenga misikiti katika maeneo hayo.”
Huu ndio mwisho wa yale ambayo Allaah (Ta´ala) ametuwezesha kuyakusanya kuhusu “Ahkaam-ul-Janaa-iz”.
Dameski 1/7/1373
Imeandikwa upya jioni ya jumapili 19/4/1382
Sifa zote njema anastahiki Allaah, Mola wa walimwengu.
- Muhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz wa Bid´ahaa, uk. 299-301
- Imechapishwa: 16/08/2026

Muhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz wa Bid´ahaa, uk. 299-301
Imechapishwa: 16/08/2026
https://firqatunnajia.com/146-kufaa-kuchimbua-makaburi-ya-makafiri-ikihitajika/