Tunafaidika yafuatayo kutokana na Hadiyth:
1 – Uharamu wa kuchimbua kaburi la muislamu kwa sababu ndani yake kuna khatari ya kuvunjika kwa mifupa yake. Kwa sababu hiyo baadhi ya Salaf walikuwa na tahadhari kuchimbiwa kaburi katika makaburi ambayo tayari kuna watu wengi waliozikwa. Imaam ash-Shaafi´iy amesema katika “al-Umm” (1/245):
“Maalik ametukhabarisha, kutoka kwa Hishaam bin ´Urwah, kutoka kwa baba yake ambaye amesema: ”Sipendi kuzikwa katika al-Baqiy´. Bali kuzikwa sehemu nyingine kunapendeza zaidi kwangu. Hakika anayezikwa hapo ni mmoja wa watu wawili: ama ni dhalimu, hivyo sipendi kuwa jirani yake, au ni mwema, basi sipendi mifupa yake ichimbuliwe.” Akasema: ”Ikiwa mifupa ya maiti itachimbuliwa ningependa irejeshwe ikazikwe tena.”
an-Nawawiy amesema katika “al-Majmuu´” (5/303) maneno ambayo ufupi wake ni kama ifuatavyo:
“Haijuzu kuchimbua kaburi pasi na sababu ya Kishari´ah kwa maafikiano ya wanazuoni. Hata hivyo inajuzu kwa sababu za Kishari´ah, kama yale yaliyotangulia katika masuala ya 109. Mukhtaswari wake ni ufuatao: inajuzu kulichimbua kaburi endapo maiti ameoza kabisa na akawa udongo. Wakati huo inajuzu kumzika mwingine humo. Vilevile inajuzu kulima ardhi hiyo na kujenga juu yake, kila namna ya kunufaika nayo na kuitumia kwa maafikiano ya wanazuoni. Yote haya ni kwa sharti kwamba hakuna mabaki yoyote ya maiti kama mfupa au vinginevyo, jambo ambalo hutofautiana kulingana na miji na ardhi. Linategemea maoni ya watu wa uzoefu katika hilo.”
Kutokana na hilo utajifunza uharamu wa kitendo cha baadhi ya serikali za Kiislamu kuchimba baadhi ya makaburi ya Kiislamu kwa ajili ya mipango ya ujenzi wa miji, bila kujali heshima yake wala kukatazwa kuikanyaga, kuvunja mifupa yake na mfano wa hayo. Wala asidhanie yeyote kuwa mipango hiyo ya ujenzi ina uhalali wa kufanya uhalifu huu, hapana. Hakika hiyo si katika mambo ya dharurah, bali ni ya kimaendeleo tu ambayo hayaruhusu kukiuka heshima wafu. Basi walio hai wanapaswa kupanga mambo yao pasi na kuwaudhi waliokufa.
Miongoni mwa mambo ya ajabu yanayovutia fikira ni kuona serikali hizi zinaheshimu mawe na majengo yaliyosimamishwa juu ya baadhi ya maiti zaidi kuliko heshima kwa maiti wenyewe. Kwani ikiwa mojawapo ya majengo hayo kama vile vumbi, vibanda au makanisa vinakuwa kizuizi katika mipango yao ya ujenzi, basi wanaviacha kama vilivyo na hata kurekebisha ramani ya mipango ili viendelee kubaki kwa kuwa wao wanaviona kuwa ni “mabaki ya kihistoria”. Ama makaburi yenyewe ya maiti hawayaoni kuwa yana thamani ya kupewa ulinzi kama huo. Bali baadhi ya serikali hizo – kutokana na tunavyojua – hufanya juhudi ya kuhamishia makaburi nje ya miji na kuzuia maziko katika makaburi ya zamani, jambo ambalo ni makosa mengine kwa mtazamo wangu, kwa sababu inawanyima waislamu Sunnah ya kuyatembelea makaburi. Kwa sababu si rahisi kwa watu wa kawaida kuvuka umbali mrefu kufika huko na kuweza kuyazuru na kuwaombea du´aa waliokufa. Kichocheo cha makosa haya – kwa dhana yangu – si kingine bali ni kufuata kipofu Ulaya ya kimaada isiyoamini, ambayo inalenga kufuta kila alama ya kuamini Aakhirah na kila kinachokumbusha kuhusu Aakhirah. Si kama wanavyodai eti kwa “kulinda afya”. Lau hilo lingekuwa kweli, basi wangeanza kupambana na mambo ambayo hakuna mwenye akili anayetilia shaka madhara yake, kama vile uuzaji wa pombe, unywaji wake, ufasiki na ufuska kwa kila namna na jina. Basi kutojali kwao kutokomeza maovu haya ya wazi na kujitahidi kwao kuondoa kila kilicho na ukumbusho kuhusu Aakhirah na kukivua mbali na macho yao ni dalili kubwa kuwa nia yao si kama wanavyodai na kutangaza, bali yale yanayofichwa ndani ya vifua vyao ni makubwa zaidi.
2 – Hakuna heshima kwa mifupa ya wasiokuwa waumini, kwa sababu ya kule kuambatanishwa neno “mfupa” kwa muumini katika maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
”… mfupa wa muumini.”
Hilo likaashiria kwamba mfupa wa kafiri si hivyo. Ameashiria maana hii Haafidhw katika “al-Fath” aliposema:
“Tunafaidika ya kuwa heshima ya muumini baada ya kufa kwake bado ipo kama ilivyokuwa akiwa hai.”[1]
Kutokana na hilo hujibiwa swali ambalo huulizwa mara kwa mara na wanafunzi wengi katika vyuo vya tiba, nalo ni: Je, inajuzu kuvunja mifupa kwa ajili ya kuichunguza na kufanya majaribio ya kitabibu? Jibu ni kwamba haijuzu kufanya hivyo kwa mifupa ya muumini, na inajuzu kwa nyinginezo zisizo za waumini. Hili linaungwa mkono na yanayokuja katika masuala yanayofuata:
[1] Ameyataja katika ”Faydhw” (4/551).
- Muhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz wa Bid´ahaa, uk. 297-299
- Imechapishwa: 16/08/2026

Muhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz wa Bid´ahaa, uk. 297-299
Imechapishwa: 16/08/2026
https://firqatunnajia.com/145-faida-mbili-kutokana-na-yaliyotangulia/