Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:
119 – Watenda madhambi makubwa wa ummah wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hawatodumishwa Motoni milele pale watapokufa hali ya kuwa ni wapwekeshaji.
MAELEZO
Madhambi makubwa ni yale madhambi yaliyo chini ya shirki na yanakuwa juu ya madhambi madogo. Kigezo cha madhambi makubwa ni kila dhambi ambayo inapelekea kuadhibiwa, ghadhabu, kulaaniwa, Moto au Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akajitenga mbali na yule mtendaji. Mfano wa madhambi makubwa ni pale ambapo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema:
”Yule mwenye kutufanyia ghushi basi si katika sisi, na yule mwenye kubeba silaha dhidi yetu si katika sisi.”[1]
Mambo yote haya yanajulisha kuwa dhambi hiyo ni kubwa, lakini hata hivyo ni chini ya shirki. Mwenye nayo hatoki nje ya imani. Ima anazingatiwa kuwa ni muumini mwenye imani pungufu au anaitwa kuwa ni fasiki. Hii ndio ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Hawakufurishi kwa madhambi makubwa yaliyo chini ya shirki, kama ambavyo hawawazingatii wenye nayo kuwa ni waumini wenye imani kamilifu. Badala yake wanawazingatia kuwa ni waumini kutokana na imani yao na ni mafasiki kutokana na madhambi yao makubwa. Ni kosa kuwazingatia watenda madhambi makubwa kuwa ni waumini wenye imani kamili, kama wanavofanya Murji-ah. Ni kosa pia kuwatoa nje ya Uislamu, kama wanavofanya Khawaarij na Mu´tazilah.
[1]al-Bukhaariy (6874) na Muslim (101).
- Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 154-155
- Imechapishwa: 24/11/2024
Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:
119 – Watenda madhambi makubwa wa ummah wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hawatodumishwa Motoni milele pale watapokufa hali ya kuwa ni wapwekeshaji.
MAELEZO
Madhambi makubwa ni yale madhambi yaliyo chini ya shirki na yanakuwa juu ya madhambi madogo. Kigezo cha madhambi makubwa ni kila dhambi ambayo inapelekea kuadhibiwa, ghadhabu, kulaaniwa, Moto au Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akajitenga mbali na yule mtendaji. Mfano wa madhambi makubwa ni pale ambapo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema:
”Yule mwenye kutufanyia ghushi basi si katika sisi, na yule mwenye kubeba silaha dhidi yetu si katika sisi.”[1]
Mambo yote haya yanajulisha kuwa dhambi hiyo ni kubwa, lakini hata hivyo ni chini ya shirki. Mwenye nayo hatoki nje ya imani. Ima anazingatiwa kuwa ni muumini mwenye imani pungufu au anaitwa kuwa ni fasiki. Hii ndio ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Hawakufurishi kwa madhambi makubwa yaliyo chini ya shirki, kama ambavyo hawawazingatii wenye nayo kuwa ni waumini wenye imani kamilifu. Badala yake wanawazingatia kuwa ni waumini kutokana na imani yao na ni mafasiki kutokana na madhambi yao makubwa. Ni kosa kuwazingatia watenda madhambi makubwa kuwa ni waumini wenye imani kamili, kama wanavofanya Murji-ah. Ni kosa pia kuwatoa nje ya Uislamu, kama wanavofanya Khawaarij na Mu´tazilah.
[1]al-Bukhaariy (6874) na Muslim (101).
Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 154-155
Imechapishwa: 24/11/2024
https://firqatunnajia.com/145-waislamu-watenda-madhambi-hawatodumishwa-motoni-milele/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)