al-´Ayyaashiy amesema kuhusiana na maneno ya Allaah:
فَأَذَّنَ مُؤَذِّنٌ بَيْنَهُمْ أَن لَّعْنَةُ اللَّـهِ عَلَى الظَّالِمِينَ
“Basi mtangazaji atatangaza baina yao kwamba: “Laana ya Allaah iwe juu ya madhalimu.”[1]
“Mas´adah bin Swadaqah amepokea kutoka kwa Ja´far bin Muhammad, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa ´Aliy ambaye amesema:
“Mimi ndiye kigogo wa waumini. Mimi ndiye mtanguliaji wa mwanzo, khaliyfah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), mimi ndiye mwenye kugawa Pepo na Moto na mimi ndiye ambaye nitasimama mlimani kati ya Pepo na Moto.”[2]
Allaah amemtakasa ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anh) kutokamana na madai haya ya kijinga na ya kipumbavu. Kwani madai haya yanafahamisha kwamba ´Aliy ni mbora kuliko waumini wengine wote wakiwemo Mitume watukufu. Madai haya yanaangusha vilevile ukhaliyfah mwongofu ambao ´Aliy alikula kiapo cha utiifu kwa kutaka kwake mwenyewe. Alikubali mwenyewe kuwa Abu Bakr na ´Umar ni wabora kuliko yeye.
Kusema kwamba yeye ndiye anawagawa watu wa kwenda Peponi na Motoni ni uongo uliokolea na madai ambayo maana yake ni kwamba yeye ni mshirika wa Allaah katika jambo hilo.
Kusema kwamba yeye ndiye ambaye atasimama mlimani kati ya Pepo na Moto kunapingana na Aayah isemayo:
وَنَادَىٰ أَصْحَابُ الْأَعْرَافِ
“Watu wa al-A´raaf watawaita… “[3]
Ni watu wengi na si mtu mmoja. Ni jambo linapingana vilevile na uongo unaokuja ambao unanasibishwa kwa Salmaan.
[1] 07:44
[2] Tafsiyr al-´Ayyaashiy (2/18).
[3] 07:48
- Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 199-200
- Imechapishwa: 12/09/2018
al-´Ayyaashiy amesema kuhusiana na maneno ya Allaah:
فَأَذَّنَ مُؤَذِّنٌ بَيْنَهُمْ أَن لَّعْنَةُ اللَّـهِ عَلَى الظَّالِمِينَ
“Basi mtangazaji atatangaza baina yao kwamba: “Laana ya Allaah iwe juu ya madhalimu.”[1]
“Mas´adah bin Swadaqah amepokea kutoka kwa Ja´far bin Muhammad, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa ´Aliy ambaye amesema:
“Mimi ndiye kigogo wa waumini. Mimi ndiye mtanguliaji wa mwanzo, khaliyfah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), mimi ndiye mwenye kugawa Pepo na Moto na mimi ndiye ambaye nitasimama mlimani kati ya Pepo na Moto.”[2]
Allaah amemtakasa ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anh) kutokamana na madai haya ya kijinga na ya kipumbavu. Kwani madai haya yanafahamisha kwamba ´Aliy ni mbora kuliko waumini wengine wote wakiwemo Mitume watukufu. Madai haya yanaangusha vilevile ukhaliyfah mwongofu ambao ´Aliy alikula kiapo cha utiifu kwa kutaka kwake mwenyewe. Alikubali mwenyewe kuwa Abu Bakr na ´Umar ni wabora kuliko yeye.
Kusema kwamba yeye ndiye anawagawa watu wa kwenda Peponi na Motoni ni uongo uliokolea na madai ambayo maana yake ni kwamba yeye ni mshirika wa Allaah katika jambo hilo.
Kusema kwamba yeye ndiye ambaye atasimama mlimani kati ya Pepo na Moto kunapingana na Aayah isemayo:
وَنَادَىٰ أَصْحَابُ الْأَعْرَافِ
“Watu wa al-A´raaf watawaita… “[3]
Ni watu wengi na si mtu mmoja. Ni jambo linapingana vilevile na uongo unaokuja ambao unanasibishwa kwa Salmaan.
[1] 07:44
[2] Tafsiyr al-´Ayyaashiy (2/18).
[3] 07:48
Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 199-200
Imechapishwa: 12/09/2018
https://firqatunnajia.com/142-al-ayyaashiy-upotoshaji-wake-wa-sita-wa-al-araaf/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)