Katika Hadiyth hizi kuna uharamu wa kusafiri kuelekea sehemu yoyote ya sehemu zilizobarikiwa, kama makaburi ya Manabii na waja wema. Hata kama maneno yake yamekuja kwa tamko la kukanusha:
”Msifunge safari… ”
makusudio ni katazo, kama alivyosema Haafidhw, kwa mfano wa maneno Yake (Ta´ala):
فَلَا رَفَثَ وَلَا فُسُوقَ وَلَا جِدَالَ فِي الْحَجِّ
”… basi asifanye tendo la ndoa wala ufasiki wala mabishano katika hijjah.”[1]
Vilevile ni kama alivyosema at-Twaybiy:
“Hii ni kali zaidi kuliko katazo la moja kwa moja. Ni kama kwamba amesema: ”Haistahiki kabisa mtu akakusudia matembezi kwa sehemu nyingine isipokuwa hizi sehemu tatu kwa ajili ya heshima zake maalum walizopewa.”
Miongoni mwa yanayounga mkono kuwa kukanusha hapa ni kwa maana ya katazo ni riwaya ya Muslim katika Hadiyth ya pili yenye tamko lisemalo:
“Msifunge safari… ”
Kisha Haafidhw akasema:
”Maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
”… isipokuwa kuelekea misikiti mitatu… ”
ubaguzi hapa ni mtupu na tafsiri yake ni kwamba haifai kufunga safari kwenda sehemu yoyote. Matokeo yake ni makatazo ya kusafiri kuelekea sehemu yoyote isipokuwa hizo tatu, kwa kuwa sehemu inayotolewa kutoka kwake katika upendeleo mtupu huwa inakisiwa kwa maana ya jumla ya jumla zote. Lakini inawezekana kuwa makusudio ya jumla hapa ni maalum, kwa maana ya misikiti tu.”
Uwezekano huu ni dhaifu na sahihi ni tafsiri ya kwanza. Kwa sababu ilivyotangulia katika Hadiyth ya Abu Baswrah na Ibn ´Umar ya kukemea safari kuelekea Ṭuwr, jambo ambalo itakuja bayana yake.
Kisha Haafidhw akasema:
“Katika Hadiyth hii kuna fadhilah za misikiti hii mitatu na ubora wake juu ya mingine kwa kuwa ni misikiti ya Manabii. Jengine ni kwa sababu wa kwanza ndio Qiblah cha watu na wanahiji kuelekea huko, cha pili kilikuwa Qiblah cha mataifa yaliyopita na cha tatu ni cha msikiti uliojengwa juu ya kumcha Allaah.”
Akaendelea kusema:
“Aidha wamekhitilafiana kuhusu kufunga safari kuelekea maeneo mengine, kama vile kumtembelea mtu mwema akiwa hai au mfu au kwenda maeneo yenye fadhilah kwa ajili ya kupata baraka na kuswali maeneo hayo. Shaykh Abu Muhammad al-Juwayniy[2] amesema:
”Ni haramu kufunga safari kuelekea sehemu nyingine yoyote isipokuwa hii misikiti mitatu kwa kufuata dhahiri ya Hadiyth.”
al-Qaadhwiy Husayn ameashiria chaguo lake na hivyo ndivo alivyosema ´Iyaadhw na kundi lake. Linalounga mkono hili ni yale waliyopokea watunzi wa ”as-Sunan” kuhusu makemeo ya Abu Baswrah al-Ghifaariy kwa Abu Hurayrah kutokana na kutoka kwake kwenda Ṭuwr na akamwambia:
”Lau ningekupata kabla hujatoka, basi usingetoka.”
Akajengea hoja kwa Hadiyth hii. Kwa hiyo ikafahmisha ya kwamba anaona kuwa anaona kuwa Hadiyth hiyo inabeba maana yake kwa ujumla na Abu Hurayrah akaafikiana naye. Maoni sahihi kwa Imam al-Haramayn na wengineo katika ash-Shaafi´iyyah ni kwamba si haramu. Hadiyth wameitolea majibu yafuatayo:
1 – Miongoni mwake ni kuwa makusudio ni kwamba fadhilah kamili ipo katika kufunga safari kuelekea misikiti hii mitatu tu, tofauti na mingine ambapo inafaa lakini hayana fadhilah hiyo kamili. Imekuja katika upokezi wa Ahmad utakaotajwa baadaye kwa tamko lisemalo:
”Hawaendeshwi wanyama wa safari isipokuwa…”
Tamko ambalo udhahiri wake si uharamu.”
2 – Miongoni mwake majibu yao ni kuwa katazo hili limehusishwa na yule aliyeweka nadhiri juu ya nafsi yake kuswali katika msikiti mmojawapo kati ya misikiti isiyokuwa mitatu, basi haitamlazimu kutekeleza nadhiri hiyo. Hili limeelezwa na Ibn Battwwal.
3 – Miongoni mwake ni kuwa makusudio ni hukumu ya misikiti tu na kwamba hakufungwi safari kwenda msikiti wowote kwa ajili ya kuswali humo isipokuwa misikiti mitatu hii, lakini kusudio la kwenda sehemu nyingine zisizo misikiti kwa ajili ya kumtembelea mtu mwema, jamaa, rafiki, kutafuta elimu, kufanya biashara au pikniki, basi halimo ndani ya katazo hili. Linaungwa mkono na yale aliyopokea Ahmad kwa njia ya Shahr bin Hawshab amabye amesema: Nimemsikia Abu Sa’iyd – ambaye ilitajwa kwake swalah katika Twur – ambapo akasema kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) amesema:
”Haifai kwa mwenye kupanda wanyama wa safari kufunga safari kuelekea msikiti mwingine kwa ajili ya swalah isipokuwa msikiti Mtakatifu, msikiti wa al-Aqswaa na msikiti wangu.”
Shahr ni mzuri katika Hadiyth, ingawa ndani yake kuna baadhi ya unyonge.”
Haafidhw (Rahimahu Allaah) amekuwa mwepesi mno katika kusema kuwa Shahr ni mzuri katika Hadiyth, iliha yeye mwenyewe amesema katika ”at-Taqrib:
“Ni mwenye makosa mengi.”
Hayo yametangulia hapo awali. Ni jambo linalojulikana kuwa mtu mwenye hali kama hii basi Hadiyth yake ni dhaifu na hajengewi hoja, kama alivyobainisha Haafidhw mwenyewe katika ”Sharh-un-Nukhbah.” Kisha hata tukikubali kuwa Hadiyth yake ni nzuri, hilo ni katika hali ya kutokuwa na ukinzani. Ama hapa Shahr amekinzana na masimulizi wote waliopokea Hadiyth hii kutoka kwa Abu Sa’iyd, pamoja na wengine waliopokea kutoka kwa Maswahabah wengine, kama ilivyotangulia kubainishwa. Basi vipi Hadiyth yake itakuwa nzuri ilihali imekinzana namna hii? Hakika hii ni Hadiyth dhaifu na yenye kupingana na zilizo Swahiyh pasi na shaka yoyote. Zaidi ya hayo maneno yake katika Hadiyth yasemayo:
“… kwenda msikitini.”
hayakuthibiti kutoka kwa Shahr mwenyewe. Kwani imepokelewa kutoka kwake na ´Abdul-Hamid, lakini haikupokelewa kutoka kwake na Layth bin Abiy Suliym. Riwaya ya Layth ni bora kwa kuwa inaafikiana na riwaya za wenye kuaminika, kama ulivyokwishafahamu. Vilevile anayechunguza katika Hadiyth hii atapata dalili nyingine ya kubatilika kwa kuongeza kwao maneno haya, nayo ni kuwa Abu Sa’iyd al-Khudriy alijengea hoja dhidi ya Shahr kwa sababu ya kwenda kwake Twur. Basi kama ndani ya Hadiyth ingekuwepo ongezeko hili linalohusisha hukumu kwa misikiti tu bila maeneo mengine yenye fadhilah, basi isingeliruhusiwa kwa Abu Sa’iyd kutumia Hadiyth hiyo kumkataza, kwa sababu Twur si msikiti, bali ni mlima mtukufu ambao Allaah alimzungumzisha Muusa. Basi Hadiyth hii isingelimuhusu iwapo ongezeko hilo lingekuwa sahihi. Hoja ya Abu Sa’iyd kwa Hadiyth hiyo, katika hali kama hii, ingekuwa ni makosa ya wazi ya uelewa ambayo haifai Shahr na waliokuwa naye waikubali kimya. Hivyo basi mambo haya yote yanathibitisha ubatilifu wa ongezeko hili na kwamba haina msingi wowote kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).
Kwa hiyo yaliyotangulia yanathibitisha kuwa hakuna dalili inayoweza kuhusisha Hadiyth hii na misikiti tu. Kwa hiyo yanayopasa ni kubaki juu ya kuenea kwake, kama alivyoona Abu Muhammad al-Juwayniy na waliotajwa pamoja naye, jambo ambalo ndio haki.
Sasa limebaki jukumu letu kujibu hoja yao ya kwanza na ya pili. Nasema yafuatayo:
1 – Hoja hii imeanguka kwa sababu mbili:
Ya kwanza: Ni kuwa tamko walilojengea hoja ”Haifai… ” halijathibiti katika Hadiyth, kwani amelipokea peke yake Shahr, naye ni dhaifu, kama tulivyokwishabainisha.
Ya pili: Hata tukikubali kuwa ni tamko lililothibiti, hatujisalimishi kuwa ina maana ya kutokuwa haramu. Bali kinyume chake ndio sahihi. Dalili zipo nyingi kutoka Qur-aan na Sunnah. Nitataja baadhi tu:
1 – Amesema (Ta´ala):
قَالُوا سُبْحَانَكَ مَا كَانَ يَنبَغِي لَنَا أَن نَّتَّخِذَ مِن دُونِكَ مِنْ أَوْلِيَاءَ
”Watasema: ”Utakasifu ni Wako! Haikutupasa sisi kufanya badala Yako walinzi wowote.”[3]
2 – Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Haifai yeyote kuadhibu kwa Moto isipokuwa Mola wa Moto.”
Ameipokea Abu Daawuud (2675) kupitia kwa Ibn Mas’uud na al-Daarimiy (2/222) kupitia kwa Abu Hurayrah.
3 –
“Haifai kwa mtu mkweli kuwa mtu wa kulaani.”
Ameipokea Muslim.
4 –
“Hakika swadaqah haifai kwa familia yake Muhammad.”
Ameipokea Muslim.
5 –
“Haifai kwa mja kusema: ”Mimi ni bora kuliko Yuunus bin Mattaa.”
Ameipokea al-Bukhaariy.
Ya tatu: Hata tukikubali kuwa tamko hilo linaonyesha si haramu, basi linaashiria machukizo, jambo ambalo hawakubaliani nalo. Katika maelezo ya Muslim ya an-Nawawiy amesema:
“Maoni sahihi kwa wenzetu ni kwamba haiharamishwi wala kuchukizwa.”
Hadiyth hii ni hoja dhidi yao kwa hali zote.
2 – Jibu hili kama lililotangulia halizingatiwi, kwani hakuna dalili yoyote ya kuhusisha katazo hili na jambo maalum. Inayopasa ni kubaki katika maana ya jumla, khaswa kwa kuwa limeungwa mkono na uelewa wa Maswahabah waliopokea Hadiyth hii, kama Abu Baswrah, Abu Hurayrah, Abu ´Umar na Abu Sa´iyd – iwapo Hadiyth hiyo imethibiti kutoka kwake – kwa kuwa wote walitoa hoja ya kuzuia safari ya kwenda Twur kwa kutumia Hadiyth hiyo. Wao wana uelewa zaidi wa maana ya Hadiyth kuliko wengine. Kwa sababu hii as-Swan´aaniy amesema katika “Subul-us-Salaam” (2/251):
“Kikosi cha wananazuoni wengi wameona kuwa jambo hilo si haramu. Hata hivyo wametumia hoja kwa yasiyotosha. Wamefasiri Hadiyth hizi kwa tafsiri za mbali zisizokubalika. Si sahihi kufasiri hadi kuwe na dalili yenye nguvu inayolazimisha kufanya hivyo.”
Kisha akaongezewa katika “Fath-ul-´Allaam” (1/310):
“Hakuna dalili yoyote. Hadiyth zinazohimiza kutembelea kaburi la Mtume na fadhilah zake, hakuna hata moja iliyokuja na amri ya kusafiri kwa makusudi kwenda huko, nazo zote ni dhaifu au za kutungwa, hazifai kutumiwa kamaa dalili. Wengi wa watu hawakufahamu tofauti kati ya kutembelea kaburi na kusafiri kwenda huko, wakazipotosha maana za Hadiyth kwa upotofu bila ushahidi wowote wa kufanya hivyo.”
Kwa sababu ya upotofu huo, Shaykh as-Subkiy – Allaah atusamehe sisi na yeye – alimshutumu Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah kuwa anapinga kutembelea kaburi la Mtume (Swalla Allaahu ´alayh wa sallam), hata bila ya kufunga safari, hali ya kuwa yeye alikuwa akilikubali jambo hilo na mwenye kutaja fadhilah na adabu zake katika vitabu vyake vingi vyema[4]. Aliyebainisha ukweli huu na kupinga shutuma za as-Subkiy ni mwanachuoni mkubwa Haafidhw Muhammad bin ´Abdil-Haadiy katika kitabu chake kikubwa alichokiita “as-Swaarim al-Munky fiy ar-Raddi ´ala as-Subkiy” ambamo ametaja ndani yake maneno mengi ya Ibn Taymiyyah yanayoruhusu kutembelea kaburi la Mtume bila ya kulifungia safari. Aidha akataja ndani yake Hadiyth kuhusu fadhilah za hilo, akazizungumzia kwa kina, akabainisha udhaifu wake na za kutungwa na ndani yake mna manufaa mengine mengi ya ki-Fiqh, ki-Hadiyth na kihistoria ambacho kila mwanafunzi wa elimu anapaswa kukisoma.
Zaidi ya hayo akili timamu inakubaliana na kauli ya wale waliodai kuwa Hadiyth hii ni ya jumla katika maana yake. Kwani ikiwa Hadiyth kwa maana ya wazi inakataza kusafiri kwenda misikiti mingine tofauti na misikiti mitatu, na tunajua kuwa ´ibaadah yoyote katika msikiti ni bora kuliko sehemu nyingine yoyote. Amesema (Swalla Allaahu ´alayh wa sallam):
“Sehemu zipendwazo zaidi na Allaah ni misikiti.”
Hata kama huo msikiti huo ni ule ambao umejengwa juu ya uchaji, kama msikiti Qubaa´, ambao Mtume (Swalla Allaahu ´alayh wa sallam) amesema juu yake:
“Swalah ndani ya msikiti Qubaa´ ni kama ´Umrah.”
Mambo yakishakuwa ni hivo Hadiyth hii inakataza kwa nguvu zaidi kusafari kuelekea sehemu nyingine zisizo misikiti mitatu, khaswa ikiwa sehemu hiyo imejengwa juu ya kaburi la Mtume au mja mwema kwa lengo la kuswali ndani yake na kufanya ´ibaadah mahali hapo. Tayari tunajua kuwa kuna laana kwa anayefanya hivyo. Basi je, inaingia akilini kuwa Shari´ah yenye hakima iruhusu kusafiri kwenda sehemu kama hiyo na wakati huohuo ikataze kusafari ya kwenda msikiti Qubaa´?
[1] 02:197
[2] Naye ni ´Abdullaah bin Yuusuf ambaye ni mwanachuoni wa ash-Shaafi´iyyah na baba yake Imaam al-Haramayn ´Abdul-Malik bin ´Abdillaah. Alikuwa imamu wa tafsiri ya Qur-aan, Fiqh na adabu. Alikufa mnamo 438.
[3] 25:18
[4] Kama vile kitabu chake ”Manasik-ul-Hajj” (3/390) kutoka katika ”Majmuu’at-ur-Rasaa-il al-Kubraa”.
- Muhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz wa Bid´ahaa, uk. 288-293
- Imechapishwa: 13/08/2026

Muhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz wa Bid´ahaa, uk. 288-293
Imechapishwa: 13/08/2026
https://firqatunnajia.com/141-wanazuoni-kuhusu-uharamu-wa-kufunga-safari-kutembelea-kaburi/