11 – Kusafiri kuyaendea. Kuna Hadiyth kadhaa juu ya hilo:
1 – Abu Hurayrah ameeleza ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Msifunge safari isipokuwa kuelekea misikiti mitatu; msikiti Mtakatifu, msikiti wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na msikiti wa al-Aqswaa.”
Imekuja katika upokezi mwingine kutoka kwake kwa tamko lisemalo:
”Hakika husafiri tu kuelekea misikiti mitatu; msikiti wa Ka´bah, msikiti wangu na msikiti wa Ilyaa´”.
Ameipokea al-Bukhaariy kwa tamko la kwanza na Muslim kwa tamko la pili, kupitia njia nyingine kutoka kwake. Watunzi wa as-Sunan na wengineo wameipokea kupitia njia nyingine. Aidha inayo njia ya tatu kwa Ahmad (2/501) na ad-Daarimiy (1/330). Nimeitaja Hadiyth hiyo kwa mapana katika ”ath-Thamar al-Mustatwaab”.
2 – Abu Sa´iyd al-Khudriy amesimulia ya kwamba amemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:
”Msifunge safari… ”
Imekuja katika tamko jengine:
”…. msisafiri isipokuwa kuelekea misikiti mitatu; msikiti wangu huu, msikiti Mtakatifu na msikiti wa al-Aqswaa.”
Wameipokea al-Bukhaariy, Muslim na wengineo. Inayo njia nne kutoka kwake. Nimezitaja katika chanzo kilichotajwa hapo kabla na tamko jengine ni la Muslim. Njia ya nne ameipokea Shahr bin Hawshab. Kutoka kwake wawili: Mmoja wao ni Layth bin Abiy Sulaym, kutoka kwake ambaye amesema:
“Tulikutana na Abu Sa´iyd na sisi tunakusudia Ṭuwr ambapo akasema: ”Nimemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema: ”Hawaendeshwi wanyama wa safari isipokuwa…”
Mwingine ni ´Abdul-Hamiyd bin Bahraam kutoka kwake ambaye amesema:
“Nimemsikia Abu Sa´iyd al-Khudriy na ikatajwa mbele yake swalah ya Ṭuwr ambapo akasema kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema: ”Haifai kwa mwenye kupanda wanyama wa safari kufunga safari kuelekea msikiti mwingine kwa ajili ya swalah isipokuwa msikiti Mtakatifu… ”
Wameipokea wawili hao Ahmad (3/93, 64).
Shahr ni dhaifu. Yeye peke yake ndiye aliyopokea ziada hii:
”… kwenda msikiti kwa ajili ya kutaka swalah.”
Kwa hiyo ni dhaifu na yenye kupingana na Hadiyth zilizo Swahiyh, kwa sababu haikutajwa katika njia nyingine kutoka kwa Abu Sa´iyd, hata katika njia ya Layth kutoka kwa Shahr. Vivyohivyo haikupokelewa katika Hadiyth nyingine, ambazo ni nane na nyingi kati yake zina zaidi ya njia moja. Nimezinukuu zote katika ”ath-Thamar al-Mustatwaab.” Basi kutokuwepo kwa ziada hii katika chochote miongoni mwa Hadiyth hizi – licha ya wingi wake na tofauti za njia zake – ni dalili kubwa ya udhaifu wa ziada hiyo na ubatilifu wake. Ni katika kosa la Shahr bin Hawshab au mpokezi kutoka kwake ambaye ni ´Abdul-Hamiyd, kwa sababu ndani yake kuna baadhi ya unyonge upande wa kumbukumbu yake. Haafidhw amesema katika wasifu wa Shahr katika ”at-Taqriyb”:
”Ni mkweli, lakini mwenye makosa mengi.”
3 – Abu Baswrah al-Ghifaariy ameeleza:
”Alikutana na Abu Hurayrah naye akiwa anakuja ambapo akamwambia: “Umetoka wapi?” Akasema: “Nimetoka Ṭuwr na nimeswali huko.” Akasema: “Mimi lau ningekupata kabla hujaondoka usingeenda. Kwani hakika nimemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:
”Msifunge safari isipokuwa kuelekea misikiti mitatu; msikiti Mtakatifu, msikiti huu na msikiti wa al-Aqswaa.”
Ameipokea at-Twayaalisiy (1348) na Ahmad (6/7) ambaye tamko ni lake. Cheni yake ya wapokezi ni Swahiyh. Inayo kwa Ahmad njia mbili nyingine ambapo cheni ya kwanza kati ya hizo ni nzuri na ya pili ni Swahiyh. Ameipokea pia Maalik, an-Nasaa’iy na at-Tirmidhiy na akaisahihisha kutoka njia ya tatu, isipokuwa mmoja wa mapokezi alikosea katika cheni yake akaifanya kuwa ni kutoka kwa Baswrah bin Abiy Baswrah. Katika matini yake ametaja:
”Hawaendeshwi wanyama wa safari.”
4 – Qaz´ah amesimulia:
“Nilitaka kutoka kwenda Ṭuwr ambapo nikamuuliza Ibn ´Umar ambaye akasema: ”Je, hujui kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

Ameipokea al-Azraqiy katika ”Akhbaar Makkah”, uk. 304, kwa cheni ya wapokezi Swahiyh, watu wake ni watu wa Swahiyh. Sehemu yake yenye kutoka kwa Mtume ameipokea al-Haythamiy katika ”al-Majma´” (4/4) na akasema: ”Ameipokea at-Twabaraaniy katika ”al-Kabiyr” na katika ”al-Awsatw” na wanaume wake ni wenye kuaminika.”
- Muhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz wa Bid´ahaa, uk. 285-288
- Imechapishwa: 13/08/2026

Muhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz wa Bid´ahaa, uk. 285-288
Imechapishwa: 13/08/2026
https://firqatunnajia.com/140-makatazo-ya-kufunga-safari-kwenda-kutembelea-kaburi-fulani/