141. al-´Ayyaashiy upotoshaji wake wa tano wa al-A´raaf

al-´Ayyaashiy amesema:

“Muhammad bin al-Fadhwl amepokea kutoka kwa Abul-Hasan ar-Ridhwaa ambaye amesema kuhusiana na maneno Yake:

فَأَذَّنَ مُؤَذِّنٌ بَيْنَهُمْ أَن لَّعْنَةُ اللَّـهِ عَلَى الظَّالِمِينَ

“Basi mtangazaji atatangaza baina yao kwamba: “Laana ya Allaah iwe juu ya madhalimu.”[1]

“Mwenye kunadi ni kiongozi wa waumini.”[2]

Watu hawa wanawazulia watu wa nyumbani kwa Mtume. Lau tutakadiria kuwa kweli Abul-Hasan ar-Ridhwaa aliifasiri Aayah hii tukufu kwa njia iliyotajwa, basi haikubaliwi kutoka kwake isipokuwa kwa dalili kutoka katika Qur-aan au Sunnah inayofahamisha kwamba ´Aliy ametofautika kwa manzilah hii badala ya Mitume na waumini wengine wote.

[1] 07:44

[2] Tafsiyr al-´Ayyaashiy (2/17).

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 199
  • Imechapishwa: 12/09/2018