al-´Ayyaashiy amesema:
“Mansuur bin Yuunus ameeleza kutoka kwa mtu, kutoka kwa Abu ´Abdillaah ambaye amesema kuhusiana na maneno ya Allaah:
إِنَّ الَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا وَاسْتَكْبَرُوا عَنْهَا لَا تُفَتَّحُ لَهُمْ أَبْوَابُ السَّمَاءِ وَلَا يَدْخُلُونَ الْجَنَّةَ حَتَّىٰ يَلِجَ الْجَمَلُ فِي سَمِّ الْخِيَاطِ ۚ وَكَذَٰلِكَ نَجْزِي الْمُجْرِمِينَ
“Hakika wale waliozikadhibisha Aayah Zetu na wakazifanyia kiburi, hawatofunguliwa milango ya mbingu na wala hawatoingia Peponi mpaka ngamia aingie katika tundu ya sindano – hivyo ndivyo Tunavyowalipa wahalifu.”[1]
“Aayah hii imeteremka kuhusu Twalhah, az-Zubayr na wale wote walioshiriki katika vita vya ngamia.”[2]
Allaah amemtakasa Abu ´Abdillaah kutokamana na uongo huu mkubwa.
Twalhah na az-Zubayr ni miongoni mwa Maswahabah wakubwa wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), mabwana wa Muhaajiruun na ni miongoni mwa wale kumi waliobashiriwa Pepo. az-Zubayr ni miongoni mwa kakundi kalikoteuliwa na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na pia alikuwa ni binamu yake. Lakini Baatwiniyyah Raafidhwah madhalimu hawataki jengine isipokuwa kukipotosha Kitabu cha Allaah, kuwakufurisha Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kuwahukumu kudumu Motoni milele.
Aayah hii imeteremshwa katika kipindi cha Makkah. Ni vipi basi Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alilijua hilo na akawaacha waishi al-Madiynah? Ni vipi basi awaache watangamane naye safarini, katika mji na wapigane bega kwa bega pamoja naye? Ni kwa nini Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakuwakhabarisha Ummah kwamba Aayah hii imeteremshwa juu ya fulani na fulani? Ni kwa nini mambo haya makubwa yasiwezekane isipokuwa tu kwa Raafidhwah Baatwiniyyah ambao ni maadui wa Allaah, Mtume wake, Maswahabah na waumini wengine wote?
[1] 07:40
[2] Tafsiyr al-´Ayyaashiy (2/17).
- Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 198-199
- Imechapishwa: 31/08/2018

Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 198-199
Imechapishwa: 31/08/2018
https://firqatunnajia.com/140-al-ayyaashiy-upotoshaji-wake-wa-nne-wa-al-araaf/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)