139. al-´Ayyaashiy upotoshaji wake wa tatu wa al-A´raaf

al-´Ayyaashiy amesema:

“Muhammad bin Mansuur ameeleza ya kwamba alimuuliza mja mwema kuhusiana na maneno Yake Allaah:

إِنَّمَا حَرَّمَ رَبِّيَ الْفَوَاحِشَ مَا ظَهَرَ مِنْهَا وَمَا بَطَنَ

“Hakika Mola wangu ameharamisha machafu, yaliyodhihirika na yaliyofichika.”[1]

Akasema: “Qur-aan hii ina tafsiri ya wazi na iliyofichikana. Yale yote Aliyoharamisha katika Kitabu ndio ya wazi. Miongoni mwa yaliyofichikana ni wale maimamu wakandamizi. Na yale yote Aliyohalalisha katika Kitabu ndio ya wazi. Yaliyofichikana katika hayo ni wale maimamu wa haki.”[2]

Tafsiri hii ya Baatwiniyyah inapoteza maana ya Aayah. Isitoshe ni tafsiri isiyoingia akilini. Miongoni mwa mambo ya halali kunaingia vyakula, vinywaji, mavazi na vipando. Je, hivi kweli maimamu wanaingia katika aina hizi? Hakika katika tafsiri hii kuna kukichezea shere Kitabu cha Allaah na maimamu (Rahimahumu Allaah).

Tafsiri yake ya kweli ni kwamba yaliyodhihirika ni yale maasi yanayofanyika hadharani na yaliyofichika  ni yale maasi yanayofanyikwa kwa siri. Aayah iko namna hii:

قُلْ إِنَّمَا حَرَّمَ رَبِّيَ الْفَوَاحِشَ مَا ظَهَرَ مِنْهَا وَمَا بَطَنَ وَالْإِثْمَ وَالْبَغْيَ بِغَيْرِ الْحَقِّ وَأَن تُشْرِكُوا بِاللَّـهِ مَا لَمْ يُنَزِّلْ بِهِ سُلْطَانًا وَأَن تَقُولُوا عَلَى اللَّـهِ مَا لَا تَعْلَمُونَ

“Sema: “Hakika Mola wangu ameharamisha machafu, yaliyodhihirika na yaliyofichika, na dhambi na ukandamizaji pasi na haki, na kumshirikisha Allaah kwa ambayo hakukiteremshia mamlaka na kuzungumza juu ya Allaah yale ambayo hamyajui.”

[1] 07:33

[2] Tafsiyr al-´Ayyaashiy (2/16).

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 198
  • Imechapishwa: 31/08/2018