Haafidhw al-Laalakaa’iy amepokea upokezi uliotangulia katika “Sharh Usuwl I’tiqaad Ahl-is-Sunnah wal-Jamaa’ah” kupitia kwa ‘Aliy bin ar-Rabiy’ at-Tamiymiy al-Muqriy: ´Abdullaah bin Abiydiy Daawuud: Salamah bin Abiy Shabiyb ametuhadithia.
Amefanyiwa ufuatiliwaji na Bakkar bin ´Abdillaah, kutoka kwa Mahdiy bin Ja’far, kutoka kwa Maalik, pasi na kumtaja mwalimu wake Ja’far bin ‘Abdillaah.
Ibn ´Abdil-Barr ameipokea katika “at-Tamhiyd”: Muhammad bin ´Abdil-Malik ametukhabarisha: “´Abdullaah bin Yuunus ametuhadithia: Baqiyy bin Makhlad ametuhadithia: Bakkaar bin ´Abdillaah al-Qurashiy ametuhadithia: Ja´far bin Mahdiy ametuhadithia kutoka kwa Maalik bin Anas kwamba:
“Alimuuliza kuhusu maneno Yake Allaah (‘Azza wa Jall):
الرَّحْمَـٰنُ عَلَى الْعَرْشِ اسْتَوَىٰ
”Mwingi wa rehema amelingana juu ya ´Arshi.”[1]
Amelingana vipi?” Maalik akainamisha kichwa kisha akasema: ”Kulingana Kwake hakutambuliki[2], kitendo Chake ni kitu kisichofahamika na kuuliza juu ya hilo ni Bid´ah.”[3]
Amefanyiwa ufuatiliwa na Imaam ad-Daarimiy, ambaye amesema katika kitabu chake “ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah”: Mahdiy bin Ja’far ar-Ramliy ametuhadithia: Ja’far bin ´Abdillaah – ambaye alikuwa ni katika Ahl-ul-Hadiyth na alikuwa ni mtu madhubuti . ametuhadithia, kutoka kwa mtu ambaye alinitajia jina lake:
“Bwana mmoja alikuja kwa Maalik bin Anas…”[4]
Aliongeza mtu baada ya Ja´far bin ‘Abdillah.
Mahdiy bin Ja’far alikuwa mkweli lakini mwenye kukosea. Amesimulia kisa hiki kwa njia tofauti. Mara amekisimulia kutoka kwa mwalimu wake Ja’far bin ‘Abdillaah, kutoka kwa Maalik. Wakati mwingine amekisimulia kutoka kwa mwalimu wake Ja’far bin ‘Abdillaah, kutoka kwa bwana mmoja, kutoka kwa Maalik. Mara ya tatu amekisimulia moja kwa moja kutoka kwa Maalik. Walakini tofauti hii kutoka katika njia hii haipingani na kusihi kwa kisa, kwa sababu imesimuliwa kutoka njia zingine ambazo zinaisapoti na kuitia nguvu.
[1] 20:05
[2] Namna hii ndivo umepokelewa upokezi katika “at-Tamhiyd” na ni yakini iliyopotoshwa. Sahihi ni kwamba ni kama ilivyopokelewa katika zile njia zilizotangulia zinazosema kwamba kulingana Kwake si kitu kisichotambulika. Kisha kuna mwanafunzi mwaminifu ambaye amenizindua ya kwamba alisoma nakala ya at-Tamhiyd Marocco ambapo mwandishi aliweka ”si” katika uwanja wa maoni. Kisha mimi mwenyewe nikapigiwa picha nakala hiyo na nikagundua kuwa mambo ndivo yalivyo.
[3] at-Tamhiyd (7/149-153).
[4] ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah, uk. 55-56.
- Muhusika: Shaykh ´Abdur-Razzaaq bin ´Allaamah ´Abdil-Muhsin al-´Abbaad al-Badr
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Athar al-Mash-huur ´an-il-Imaam Maalik fiy Swifat-il-Istiwaa’, uk. 31-32
- Imechapishwa: 28/11/2025

Muhusika: Shaykh ´Abdur-Razzaaq bin ´Allaamah ´Abdil-Muhsin al-´Abbaad al-Badr
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Athar al-Mash-huur ´an-il-Imaam Maalik fiy Swifat-il-Istiwaa’, uk. 31-32
Imechapishwa: 28/11/2025
https://firqatunnajia.com/14-usimuliaji-tofauti-wa-mahdiy-bin-jafar-masimulizi-ya-maalik/