Masimulizi ya Imaam Maalik (Rahimahu Allaah) yamepata umaarufu mkubwa. Jopo kubwa kutoka katika wanafunzi wameyapokea kutoka kwake kupitia njia nyingi. Yameahidiwa na kukubaliwa na wanazuoni na yamesimuliwa katika vitabu vingi vya ´Aqiydah. Hapa kutafuatia zile njia nilizozipata, ambazo yamesimulia masimulizi haya, vyanzo vyake pamoja na maneno ya wanazuoni katika kuyathibitisha kwake.
1 – Upokezi wa Ja’far bin ´Abdillaah[1].
Haafidhw Abu Nu’aym amesema: Muhammad bin ‘Aliy bin Muslim al-Uqayliy ametuhadithia: Abu Umayyah al-Ghulaabiy ametuhadithia: Salamah bin Shabiyb[2] ametuhadithia: Mahdiy bin Ja’far[3] ametuhadithia: Ja’far bin `Abdillaah ametuhadithia:
”Tulikuwa kwa Maalik bin Maalik wakati ambapo alikuja bwana mmoja na kusema: ”Ee Abu ´Abdillaah!
الرَّحْمَـٰنُ عَلَى الْعَرْشِ اسْتَوَىٰ
”Mwingi wa rehema amelingana juu ya ´Arshi.”
Amelingana vipi?”
Sijawahi kumuona Maalik anachukulia vibaya kama alivofanya siku hiyo. Akainamisha kichwa kitambo kirefu na akaanza kuchimba ardhini na kijiti chake mpaka akaanza kutokwa na jasho. Kisha akainua kichwa chake, akatupa kijiti kile na kusema: ” “Namna haifahamiki. Kulingana juu si kwamba hakufahamiki. Ni wajibu kuliamini hilo na kuuliza juu yake ni Bid´ah. Mimi sikuoni vyengine isipokuwa mzushi.” Halafu akaamrisha akatolewa nje.”[4]
Imaam Abu Ismaa´iyl as-Swaabuuniy (Rahimahu Allaah) amepokea na kusema: Abu Muhammad al-Makhladiy ametukhabarisha: Abu Bakr ´Abdullaah bin Muhammad bin Muslim al-Isfaaraayiyniy ametuhadithia: Abul-Husayn al-Hasaniy ametuhadithia: Salamah bin Shabiyb ametuhadithia: Mahdiy bin Ja´far bin Maymun ar-Ramliy ametuhadithia kutoka kwa Ja´far bin ´Abdillaah:
”Bwana mmoja alikuja kwa Maalik bin Anas akasema: ”Ee Abu ´Abdillaah:
الرَّحْمَـٰنُ عَلَى الْعَرْشِ اسْتَوَىٰ
”Mwingi wa rehema amelingana juu ya ´Arshi.”[5]
Amelingana vipi?”
Sijapatapo kumuona Maalik akichukulia vibaya kabisa kama mara hiyo. Akaanza kutokwa na jasho na huku watu wanasubiri wasikie atachosema. Kisha akajivuta na kusema:
”Namna si kitu kisichojulikana. Kulingana haitambuliki. Ni wajibu kuamini hilo na ni Bid´ah kuulizia hilo. Nachelea ukawa mpotevu.” Kisha akaamrisha atolewe nje.”[6]
Imaam as-Swaabuuniy amepokea pia kupitia njia nyingine: Babu yangu pia Abu Haamid Ahmad bin Ismaa´iyl amenikhabarisha nayo, kutoka kwa babu yangu mkubwa na shahidi Abu ´Abdillaah Muhammad bin ´Adiy bin Hamduuyah as-Swaabuuniy: Muhammad bin Ahmad bin Abiy ´Awn an-Nasawiy ametuhadithia: Salamah bin Shabiyb ametuhadithia: Mahdiy bin Ja’far ar-Ramliy ametuhadithia: Ja’far bin ´Abdillaah ametuhadithia:

”Mwingi wa rehema amelingana juu ya ´Arshi.”[7]
Amelingana vipi?”
Sijapatapo kumuona Maalik akichukulia vibaya kabisa kama mara hiyo… ”[8]
[1] adh-Dhahabiy amemjumuisha na wasimulizi wa Maalik wenye majina yanayofanana, ambapo Ibn Naaswir-id-Diyn akamraddi na kusema:
“Ni jambo linahitaji kuangaliwa vyema. Kw sababu kusema hivo kwa kuachia kunatoa hisia fulani kwamba Imaam Maalik bin Anas alikuwa mwalimu wa Ja´far, kama vile mtunzi anaonelea hivo. Hiyo si kweli. Badala yake alikuwa ni yule Maalik bin Khaalid al-Asdiy al-Baswriy, kama alivyomwita hivo al-Aamiyr na wengineo.” (Tawdhwiyh-ul-Mushtabih (4/98-99))
Ibn Hajar amesema hayohayo katika “Tabswiyr-ul-Muntabih” (2/621).
[2] Abu ´Abdir-Rahmaan Salamah bin Shabiyb an-Naysaabuuriy al-Hajriy al-Masma´iy, aliyekuwa akiishi Makkah. Abu Haatim amesema kwamba alikuwa ”mkweli” ilihali Abu Nu´aym amesema “mmoja katika wakweli ambaye maimamu na wazee wamehadithia kutoka kwake”. Alifariki mnamo 247. Tazama “Tahdhiyb-ul-Kamaal” (11/284).
[3] Abu Muhammad Mahdiy bin Ja´far bin Jayhaan bin Bahraam ar-Ramliy. Ibn Hajar amesema “mkweli mwenye kuksoea”. Tazama “Taqriyb-ut-Taqriyb” (6979). Ibn Hajar amemnukuu adh-Dhahabiy ambaye amesema:
“Nimeona kuwa anasimulia kutoka kwa Maalik katika ”Tafsiri ya Qur-aan” ya Ibn Abiy Haatim.” (Tahdhiyb-ut-Tahdhiyb (10/289))
Alifariki mnamo 230.
[4] Hilyat-ul-Awliyaa’ (8909) na adh-Dhahabiy katika “Siyar A´laam-in-Nubalaa’” (8/100) kupitia kwa Abu Nu´aym.
[5] 20:05
[6] ´Aqiydat-us-Salaf wa Asw-haab-il-Hadiyth, uk. 38.
[7] 20:05
[8] ´Aqiydat-us-Salaf wa Asw-haab-il-Hadiyth, uk. 39.
- Muhusika: Shaykh ´Abdur-Razzaaq bin ´Allaamah ´Abdil-Muhsin al-´Abbaad al-Badr
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Athar al-Mash-huur ´an-il-Imaam Maalik fiy Swifat-il-Istiwaa’, uk. 29-31
- Imechapishwa: 28/11/2025

Muhusika: Shaykh ´Abdur-Razzaaq bin ´Allaamah ´Abdil-Muhsin al-´Abbaad al-Badr
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Athar al-Mash-huur ´an-il-Imaam Maalik fiy Swifat-il-Istiwaa’, uk. 29-31
Imechapishwa: 28/11/2025
https://firqatunnajia.com/13-masimulizi-ya-maalik-kwa-mujibu-wa-jafar-bin-abdillaah/