14. Qur-aan kwa mujibu wa Mu´tazilah

Mu´tazilah wanasema kuwa Qur-aan imeumbwa na kwamba maneno aliyosikia Muusa yalikuwa yanatoka kwenye mti. Wanamaanisha kuwa Allaah aliyaumba kwenye mti na kuwa sio maneno ya Allaah (Tabaarak wa Ta´ala). Wanamaanisha kuwa maneno ya Allaah hayakuacha kuwa ni yenye kuumbwa. Huku ni kumsemea Allaah uongo na ni kuzungumza juu ya Allaah pasi na elimu:

قُلْ إِنَّمَا حَرَّمَ رَبِّيَ الْفَوَاحِشَ مَا ظَهَرَ مِنْهَا وَمَا بَطَنَ وَالْإِثْمَ وَالْبَغْيَ بِغَيْرِ الْحَقِّ وَأَن تُشْرِكُوا بِاللَّـهِ مَا لَمْ يُنَزِّلْ بِهِ سُلْطَانًا وَأَن تَقُولُوا عَلَى اللَّـهِ مَا لَا تَعْلَمُونَ

“Sema: “Hakika hapana vyenginevyo Mola wangu ameharamisha machafu, yaliyodhihirika na yaliyofichika na dhambi [zote] na ukandamizaji bila ya haki. Na [ameharamisha] kumshirikisha Allaah kwa kile hakukiteremshia mamlaka na kusema juu ya Allaah yale ambayo hamyajui.”[1]

[1] 07:33

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Qurrat-ul-´Aynayn bi Tawdhwiyh Ma´aaniy ´Aqiydat-ir-Raaziyayn, uk. 24
  • Imechapishwa: 15/10/2016