14 – Muheshimiwa Shaykh ´Abdul-´Aziyz ar-Raajihiy (Hafidwahu Allaah)

Aliulizwa swali lifuatalo:

“Baadhi ya watu wanamtuhumu yule mwenye kushikamana barabara na mfumo wa Salaf kwamba ni “Jaamiy” na wanamtahadharisha Shaykh Rabiy´, Shaykh an-Najmiy, Shaykh Zayd bin Muhammad Haadiy al-Madkhaliy na wanachuoni wengine.

Akajibu:

Majina bandia hayageuzi kitu. Si sawa kupeana majina bandia. Kilicho umuhimu ni uzani wa mtu. Wanachuoni hao tunajua kuwa ´Aqiydah yao ni salama na kwamba ni katika Ahl-us-Sunnah. Shaykh Rabiy´, Shaykh Ahmad na Shaykh Zayd hakuna vumbi lolote juu yao.”

Pia aliulizwa swali lifuatalo:

“Unasemaje juu ya vitabu na kanda za Shaykh Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy (Hafidhwahu Allaah)? Unapendekeza kusoma vitabu vyake na kusikiliza kanda zake?

Akajibu kwa kusema:

“Ndio, hayana neno. Vitabu na kanda zake hatujaona ndani yake cha kukosoa. Hakujakosolewa kitu. Kanda zake ni nzuri na vitabu vyake ni vizuri na vyenye faida.”[1]

[1] Kanda iliorekodiwa na ”Minhaaj-is-Sunnah” Riyaadh”.

  • Mhusika: Shaykh Khaalid bin Dhwahwiy adh-Dhwafayriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.rabee.net/ar/sharticles.php?cat=12&id=57
  • Imechapishwa: 05/12/2019