Inampasa mwalimu amlee mwanafunzi hatua kwa hatua kwa adabu za Sunnah, tabia njema zinazopendeza, kuizoesha nafsi yake katika mambo madogo yaliyofichika, kumzoesha kujilinda katika mambo yake yote ya ndani na ya wazi, kumhamasisha kwa maneno yake na matendo yake yanayorudiwa juu ya kumtakasia nia Allaah, ukweli, uzuri wa nia na kumcha Allaah katika nyakati zote. Anatakiwa kumfahamisha kwamba kwa hilo zitamfungukia nuru za maarifa, kifua chake kitapanuka na zitabubujika kutoka moyoni mwake chemchem za hekima na mambo mazuri yaliyojificha, kwamba Allaah atambariki katika elimu na hali yake na ataongozwa katika matendo na maneno yake.
- Muhusika: Imaam Yahyaa bin Sharaf an-Nawawiy (afk. 677)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Tibyaan fiy Aadaabi Hamalat-il-Qur-aan, uk. 31
- Imechapishwa: 19/08/2026
Inampasa mwalimu amlee mwanafunzi hatua kwa hatua kwa adabu za Sunnah, tabia njema zinazopendeza, kuizoesha nafsi yake katika mambo madogo yaliyofichika, kumzoesha kujilinda katika mambo yake yote ya ndani na ya wazi, kumhamasisha kwa maneno yake na matendo yake yanayorudiwa juu ya kumtakasia nia Allaah, ukweli, uzuri wa nia na kumcha Allaah katika nyakati zote. Anatakiwa kumfahamisha kwamba kwa hilo zitamfungukia nuru za maarifa, kifua chake kitapanuka na zitabubujika kutoka moyoni mwake chemchem za hekima na mambo mazuri yaliyojificha, kwamba Allaah atambariki katika elimu na hali yake na ataongozwa katika matendo na maneno yake.
Muhusika: Imaam Yahyaa bin Sharaf an-Nawawiy (afk. 677)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Tibyaan fiy Aadaabi Hamalat-il-Qur-aan, uk. 31
Imechapishwa: 19/08/2026
https://firqatunnajia.com/14-malezi-ya-mwalimu/