Inampasa mwalimu asijivune juu ya wanafunzi. Bali awapolekee na ajishushe pamoja nao. Kwani kumepokelewa kuhusu unyenyekevu kwa watu mmojammoja mambo mengi yanayojulikana – basi vipi kwa hawa ambao wako kama wanawe pamoja na walivyo katika kushughulika na Qur-aan, pamoja na walivyo na haki juu yake ya usuhuba na kurudia kwao kwake? Imepokelewa kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Kuwa wapole kwa wale mnaowafundisha na kwa wale mnaojifunza kwao.”[1]

Abu Ayyuub as-Sakhtiyaaniy (Rahimahu Allaah) amesema:

”Inampasa mwanachuoni kuweka udongo juu ya kichwa chake kwa unyenyekevu kwa ajili ya Allaah (´Azza wa Jall).”

[1] Dhaifu mno kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Dhwa´iyf-ul-Jaamiy´” (2494).

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tibyaan fiy Aadaabi Hamalat-il-Qur-aan, uk. 29-30
  • Imechapishwa: 19/08/2026