Swali 14: Ni ipi hukumu ya kumuosha maiti kwa sabuni na shampoo[1]?

Jibu: Naona kuwa mfanyie kazi kile kilichomo ndani ya Hadiyth ya Umm ´Atwiyyah. Muosheni maiti kwa maji yaliyochanganyikana na mkunazi katika maosho yote. Mwanzeni vile viungo vyake vya kulia na vile viungo vyake vya wudhuu´ pamoja na kutilia umuhimu suala la kuondoa uchafu uliorundikana na mwengine katika maosho yote mpaka asafike ijapo mtazidisha mara saba kutokana na Hadiyth iliyotajwa.

Hapana haja ya sabuni, shampoo na vyenginevyo. Isipokuwa ikiwa mkunazi hautosihi katika kuondosha uchafu. Katika hali hiyo hakuna neno kutumia sabuni, shampoo na Ashnaan[2] na vyenginevo vinavoondosha uchafu kwa kuanza navyo katika muosho wa kwanza. Muosho wa mwisho ajaalie kitu katika kafura kutokana na Hadiyth iliyotajwa. Hii ndio Sunnah kutokana na tunavojua kutokana na zile Hadiyth Swahiyh kukiwemo ya ´Umm ´Atwiyyah na nyenginezo zilizopokelewa zikiwa na maana kama hiyo.

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (13/111-112).

[2] Tazama https://en.wikipedia.org/wiki/Saltwort

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz, uk. 18-19
  • Imechapishwa: 12/12/2021