9- Hedhi ni kitu chenye kuthibitisha kuwa mwanamke hana mimba. Ni kitu ambacho mtu anakihitajia kila wakati ambapo anataka kujua kuwa mwanamke ana mimba au hana.

Mfano wa hilo mwanaume amefariki na ameacha mwanamke ambaye amebeba mrithi wa mwanaume huyo. Mwanamke huyo ana mume. Asifanye naye jimaa mpaka apate hedhi au mpaka ibainike kuwa ana mimba. Ikibainika kuwa ana mimba, basi mtoto atamrithi mwanaume huyo kwa kuwa ilipatikana pindi mrithiwa alipofariki. Na akipata hedhi, basi mtoto huyo hatomrithi mwanaume huyo kwa sababu hakuwa na mimba pale alipopata hedhi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ad-Dimaa’ at-Twabiy´iyyah lin-Nisaa’ http://www.ibnothaimeen.com/all/books/article
  • Imechapishwa: 30/10/2016