14. Hadiyth “Yule atakayetawadha na kuswali kama alivyoamrishwa… “

396 – ´Aaswim bin Sufyaan ath-Thaqafiy amesema:

“Walitakikana washiriki katika vita vya mnyororo, lakini wakavikosa, ambapo badala yake wakaenda kulinda mipaka ya nchi. Kisha baadaye wakarejea kwa Mu´aawiyah, ambaye alikuwa ametembelewa na Abu Ayyuub na ´Uqbah bin ´Aamir. ´Aaswim akasema: “Ee Abu Ayyuub, tumekosa vita vya jumla. Tumepata khabari kuwa ambaye ataswali katika misikiti minne basi atasamehewa dhambi zake.” Akasema: “Ee mtoto wa kaka yangu kipenzi, hivi nisikujuze juu ya jambo ambalo ni jepesi zaidi kuliko hilo?” Hakika mimi nimemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:

مَن توضّأَ كما أُمِر، وصلَّى كما أُمِر؛ غُفر له ما قَدَّم مِن عَمل

“Yule atakayetawadha na kuswali kama alivyoamrishwa, basi atasamehewa matendo yake yaliyotagulia.”[1]

Akasema: “Mambo ni hivyo kweli, ee ´Uqbah?” Akasema: “Ndio.”

Ameipokea an-Nasaa’iy, Ibn Maajah na Ibn Hibbaan katika ”as-Swahiyh” yake.

[1] Nzuri na Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/283)
  • Imechapishwa: 31/01/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy