al-Halabiy amesema:
“Ama kuhusiana na Shaykh Ibn ´Uthaymiyn (Rahimahu Allaah), haikuthibiti kuwa Shaykh Rabiy´ amesema hivo. Lakini hata hivyo imethibiti kuwa amesema kwenye mkanda “Man hum al-Murji-ah?”:
“Niliwaambia wanafunzi wa Shaykh Qaaswim: “Je, mnajua lolote kuhusiana na Suufiyyah na Jamaa´at-ut-Tabliygh?” Wakasema: “Hapana.” Hivo nikasema: “Mkiendelea hivo kutowafahamu Suufiyyah na kuchukulia usahali kuenea kwa Ahl-ul-Bid´ah, basi bendera za Suufiyyah zitakuja kujaa kwenye moyo wa Najd badala ya bendera za Tawhiyd.”
Ni jambo lenye kujulikana kwamba Shaykh wa Qaaswim wakati ule ilikuwa ni Shaykh Ibn ´Uthaymiyn (Rahimahu Allaah). Lakini pamoja na kuwa Shaykh Rabiy´ hakumtaja kwa jina na kumlenga, hakuna yeyote mwenye haki ya kumpachika hilo na khaswa baada ya kuwa mwenyewe amekanusha hilo kwa jumla. Kwa masikitiko makubwa huu ndio usulubu wake na wapinzani wake.”[1]
1- Huu si mgongano wa batili kuwafanya watu kuelewa ya kwamba mimi namtukana ´Allaamah Ibn ´Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) kisha unajirudi mwenyewe kwa kusema:
“Lakini pamoja na kuwa Shaykh Rabiy´ hakumtaja kwa jina na kumlenga, hakuna yeyote mwenye haki ya kumpachika hilo na khaswa baada ya kuwa mwenye amekanusha hilo kwa jumla. Kwa masikitiko makubwa huu ndio usulubu wake na wapinzani wake.”?
2- Maneno hayo yanaonesha kupenda kwangu haki, kuchukia batili, kuwatakia waislamu mema na kuwatahadharisha na batili na watu wake. Ndani yake hamna kumtukana Ibn ´Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) ambaye namtukuza. Lakini kwa vile mfumo wa Salaf hauna uzito wowote kwako na wakati huo huo una ghera ya batili na watu wake ndio yanakufanya kuona haki kuwa ni batili na batili kuwa ni haki.
3- Haddaadiyyah ndio wenye kumtukana Ibn ´Uthaymiyn na Shaykh wao wa pili ndiye mwenye kumtukana Shaykh Ibn ´Uthaymiyn katika vikao vyake. Kisha ujasiri ukamshika na akaeneza maneno yake kwenye tovuti http://alathary.net/ ambapo nikayaraddi kwa makala yenye kuitwa “Daf´ Buht wa Kayd-il-Khaa-iniyn ´an-il-´Allaamah Muhammad bin ´Uthaymiyn”. Humo nimebatilisha uongo wa mwandishi huyu kuhusu ´Allaamah Ibn ´Uthaymiyn (Rahimahu Allaah).
Mimi nampenda Ibn ´Uthaymiyn na kulikuwa mapenzi makubwa kwa ajili ya Allaah baina yetu. Ni kwa nini al-Halabiy hakuchukulia kwa ubaya matusi haya? Ni kwa nini hawakemei Haddaadiyyah kwa kumtukana matusi yenye kuendelea Shaykh al-Albaaniy na kumtuhumu kwamba alikuwa na madhehebu ya Murji-ah na bali kufikia mpaka kusema kwamba alikuwa na madhehebu ya Jahmiyyah? Lakini mtu huyu ana matamanio ya upofu. Anawapiga vita watu walioshikamana na haki na kufurahishwa na batili na uongo ninaosemewa; ni vipi basi ataweza kuwakemea?
[1] Uk. 02
- Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: http://rabee.net/ar/articles.php?cat=8&id=236
- Imechapishwa: 08/01/2017

Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: http://rabee.net/ar/articles.php?cat=8&id=236
Imechapishwa: 08/01/2017
https://firqatunnajia.com/14-al-halabiy-anamtuhumu-rabiy-al-madkhaliy-kumtukana-ibn-uthaymiyn/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)