Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah amesema:

Allaah amuwie radhi Imaam Maalik bin Anas ambaye amesema:

“Kila atapotujilia mtu ambaye ni bingwa wa kubishana kuliko mwingine tuyaache yale aliyokuja nayo Jibriyl kwa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)?”[1]

MAELEZO

Huyu ni Imaam Maalik bin Anas (Rahimahu Allaah), imamu wa mji wa Uhamiaji ambaye watu walikuwa wakisafiri kwenda kwake kwa ajili ya kuchukua elimu yake, amesema:

“Kila atapotujilia mtu ambaye ni bingwa wa kubishana kuliko mwingine tuyaache yale aliyokuja nayo Jibriyl kwa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)?”

Kwa maana kwamba mwenye ubishi mwingi zaidi. Hivyo anakemea kutegemea akili, kwa sababu watu wa akili hutegemea mabishano mbalimbali. Kama Alivyosema (Ta´ala):

إِنَّكُمْ لَفِي قَوْلٍ مُّخْتَلِفٍ يُؤْفَكُ عَنْهُ مَنْ أُفِكَ قُتِلَ الْخَرَّاصُونَ

”Hakika nyinyi bila shaka mko katika kauli inayokhitilafiana. Anageuzwa kutokana na haki mwenye kugeuzwa. Wameangamia wenye kubuni uwongo.”[2]

[1] Tabwaqaat-ul-Hanaabilah (2/156).

[2] 51:8-10

  • Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaa al-Hamawiyyah, uk. 225-226
  • Imechapishwa: 15/07/2026