Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

109 – Wale wanaoswali kuelekea Qiblah haki iko kati ya mambo hayo mawili.

MAELEZO

Bi maana kati ya khofu na matarajio.

Wale wanaoswali kuelekea Qiblah wanakusudiwa waislamu. Wameitwa watu wa Qiblah kwa sababu wanaswali kuelekea Ka´bah. Kuhusu ambao hawaswali kuelekea Qiblah sio waislamu. Baada ya Allaah kufuta Shari´ah ya kuelekea Yerusalemu, akawaamrisha waislamu kuelekea Ka´bah. Kwa hiyo ni lazima kutii amri Yake (Subhaanah). Muumini anazunguka pamoja na maamrisho Yake, kwa sababu yeye ni mja:

وَمَا جَعَلْنَا الْقِبْلَةَ الَّتِي كُنتَ عَلَيْهَا إِلَّا لِنَعْلَمَ مَن يَتَّبِعُ الرَّسُولَ مِمَّن يَنقَلِبُ عَلَىٰ عَقِبَيْهِ ۚ وَإِن كَانَتْ لَكَبِيرَةً إِلَّا عَلَى الَّذِينَ هَدَى اللَّـهُ

“Hatukukifanya Qiblah ambacho ulikuwa ukikielekea isipokuwa Tupate kupambanua nani anayemfuata Mtume na nani atakayegeuka kurudi nyuma; na hakika ilikuwa ni jambo gumu isipokuwa kwa wale ambao Allaah amewaongoza.”[1]

[1]02:143

  • Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 143-144
  • Imechapishwa: 18/11/2024