Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah amesema:
Yule mwenye kupinga Kuonekana anadai kuwa akili ndio imemwelekeza kufanya hivo na ndio maana amelazimika kuipindishia maana.
MAELEZO
Mwenye kukanusha Kufufuliwa husema kwamba hakika wafu wakigeuka udongo na mifupa, basi haiwezekani warudi hai kama walivyokuwa. Wanaona kuwa hili haliwezekani kiakili. Wamempima Allaah kwa viumbe Wake. Allaah hapimwi kwa viumbe Wake, kwa sababu Yeye ni Muweza juu ya kila jambo. Yule Aliyewaumba mara ya kwanza kutoka katika kutokuwepo, je, hashindwi kuwarudisha tena?
وَهُوَ الَّذِي يَبْدَأُ الْخَلْقَ ثُمَّ يُعِيدُهُ وَهُوَ أَهْوَنُ عَلَيْهِ
”Naye ndiye aliyeanzisha uumbaji, kisha anaurudisha, nayo ni mepesi mno Kwake.”[1]
Katika kukanusha kwao Ufufuliwaji wanakanusha pia kuwepo kwa Pepo na Moto. Wanasema kwamba hakuna isipokuwa maisha ya dunia. Hakuna maisha mengine wala hakuna Pepo na Moto. Wanaona kuwa maisha yaliyopo ni ya dunia tu na kwamba ni kuishi tu na kufa:
أَيَعِدُكُمْ أَنَّكُمْ إِذَا مِتُّمْ وَكُنتُمْ تُرَابًا وَعِظَامًا أَنَّكُم مُّخْرَجُونَ هَيْهَاتَ هَيْهَاتَ لِمَا تُوعَدُونَ إِنْ هِيَ إِلَّا حَيَاتُنَا الدُّنْيَا نَمُوتُ وَنَحْيَا وَمَا نَحْنُ بِمَبْعُوثِينَ
“Je, anakuahidini kwamba nyinyi mtakapokufa mkawa mchanga na mifupa kuwa hakika mtatolewa? Mbali kabisa, mbali kabisa, Hayo mnayoahidiwa! Hakuna lolote isipokuwa tu uhai wetu wa hapa duniani tunakufa na tunahuika na wala sisi hatutofufuliwa!”[2]
Kwa maana kwamba watu fulani wanakufa na wengine wanaishi. Hii ndio imani yao kwa sababu hawaamini uwezo wa Allaah juu ya kila jambo.
[1] 30:27
[2] 23:35-37
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaa al-Hamawiyyah, uk. 223-224
- Imechapishwa: 14/07/2026
Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah amesema:
Yule mwenye kupinga Kuonekana anadai kuwa akili ndio imemwelekeza kufanya hivo na ndio maana amelazimika kuipindishia maana.
MAELEZO
Mwenye kukanusha Kufufuliwa husema kwamba hakika wafu wakigeuka udongo na mifupa, basi haiwezekani warudi hai kama walivyokuwa. Wanaona kuwa hili haliwezekani kiakili. Wamempima Allaah kwa viumbe Wake. Allaah hapimwi kwa viumbe Wake, kwa sababu Yeye ni Muweza juu ya kila jambo. Yule Aliyewaumba mara ya kwanza kutoka katika kutokuwepo, je, hashindwi kuwarudisha tena?
وَهُوَ الَّذِي يَبْدَأُ الْخَلْقَ ثُمَّ يُعِيدُهُ وَهُوَ أَهْوَنُ عَلَيْهِ
”Naye ndiye aliyeanzisha uumbaji, kisha anaurudisha, nayo ni mepesi mno Kwake.”[1]
Katika kukanusha kwao Ufufuliwaji wanakanusha pia kuwepo kwa Pepo na Moto. Wanasema kwamba hakuna isipokuwa maisha ya dunia. Hakuna maisha mengine wala hakuna Pepo na Moto. Wanaona kuwa maisha yaliyopo ni ya dunia tu na kwamba ni kuishi tu na kufa:
أَيَعِدُكُمْ أَنَّكُمْ إِذَا مِتُّمْ وَكُنتُمْ تُرَابًا وَعِظَامًا أَنَّكُم مُّخْرَجُونَ هَيْهَاتَ هَيْهَاتَ لِمَا تُوعَدُونَ إِنْ هِيَ إِلَّا حَيَاتُنَا الدُّنْيَا نَمُوتُ وَنَحْيَا وَمَا نَحْنُ بِمَبْعُوثِينَ
“Je, anakuahidini kwamba nyinyi mtakapokufa mkawa mchanga na mifupa kuwa hakika mtatolewa? Mbali kabisa, mbali kabisa, Hayo mnayoahidiwa! Hakuna lolote isipokuwa tu uhai wetu wa hapa duniani tunakufa na tunahuika na wala sisi hatutofufuliwa!”[2]
Kwa maana kwamba watu fulani wanakufa na wengine wanaishi. Hii ndio imani yao kwa sababu hawaamini uwezo wa Allaah juu ya kila jambo.
[1] 30:27
[2] 23:35-37
Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaa al-Hamawiyyah, uk. 223-224
Imechapishwa: 14/07/2026
https://firqatunnajia.com/135-ndio-maana-wakapinga-kufufuliwa/