Katika Hadiyth hizi tatu kuna dalili ya uharamu ya kuketi au kukanyaga juu ya kaburi la muislamu. Huu ndio msimamo wa kikosi kikubwa cha wanazuoni, kama alivyonukuu ash-Shawkaaniy (4/57) na wengineo. Lakini an-Nawawiy na al-‘Asqalaaniy wamenukuu kutoka kwao kwamba ni inachukiza tu. Hili la pili ndio msimamo wa Imaam ash-Shaafi‘iy katika ”al-Umm”. Vilevile imethibiti kutoka kwa Imaam Muhammad katika ”al-Aathaar”, uk. 45 ya kwamba inachukiza na akasema: ”Pia ndio msimamo wa Abu Haniyfah.”
ash-Shaafi‘iy (Rahimahu Allaah) (1/246) amesema:
”Ninakichukia kukanyaga kaburi, kuketi juu yake na kujiegemeza juu yake, isipokuwa mtu asipopata njia ya kufikia kaburi la mfu wake isipokuwa kwa kukikanyaga, basi hilo ni katika hali ya dharurah. Katika hali hiyo natumai atakuwa na ruhusa kwa idhini ya Allaah (Ta´ala). Baadhi ya wenzetu wamesema:
”Hakuna ubaya wa kuketi juu yake na kwamba alivyokataza kuketi juu yake ni kwa sababu ya kujisaidia haja kubwa. Huu si msimamo wetu, hata kama amekataza kwa sababu ya mwelekeo wa madhehebu, basi amekataza kwa ujumla wake bila kuhusianisha na madhehebu.”
ash-Shaafi‘iy (Rahimahu Allaah) alikuwa akimaanisha Imaam Maalik (Rahimahu Allaah), kwani yeye amesema waziwazi katika ”Al-Muwattwa´” kwa maana hiyo aliyoitaja. Hakuna shaka kuwa ni batili, kama alivyobainisha an-Nawawiy kwa yale aliyoyanukuu Haafidhw (3/174).
Machukizo kwao wawili yakitajwa bila kufafanuliwa basi maana yake ni uharamu. Hili liko karibu zaidi na usahihi kuliko kusema kuwa inachukiza peke yake. Haki iko katika kusema kwamba ni haramu, kwa sababu hiyo ndiyo inayosisitizwa na Hadiyth ya Abu Hurayrah na ‘Uqbah kwa kuwa ndani yake kuna onyo kali, jambo ambalo limesemwa na kundi la ash-Shaafi‘iyah akiwemo an-Nawawiy. Aidha as-Swan‘aaniy amechagua hilo katika ”Subul-us-Salaam” (1/210), Ibn Hajar al-Haytamiy amemili katika hilo katika ”az-Zawaajir” (1/143) akielekea kusema kwamba ni dhambi kubwa kutokana na yale tuliyoyaashiria ya onyo kali, jambo ambalo si mbali na usahihi.
- Muhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz wa Bid´ahaa, uk. 268-269
- Imechapishwa: 10/08/2026

Muhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz wa Bid´ahaa, uk. 268-269
Imechapishwa: 10/08/2026
https://firqatunnajia.com/135-makatazo-ya-kuketi-au-kukanyaga-juu-ya-kaburi-la-muislamu/