125 – Na ni haramu katika makaburi yafuatayo:
1 – Kuchinja kwa ajili ya Allaah. Hilo ni kutokana na maneno yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
”Hakuna kuchinja kwa ajili ya Allaah katika Uislamu.”
´Abdur-Razzaaq bin Hammaam amesema:
“Walikuwa wanachinja ng’ombe au mbuzi karibu na kaburi.”
Ameipokea Abu Daawuud (2/71), na maneno ya ´Abdur-Razzaaq ni yake pia, al-Bayhaqiy (4/57 na Ahmad (3/197) na cheni ya wapokezi ni Swahiyh kwa sharti za al-Bukhaariy na Muslim.
Shaykh-ul-Islaam amesema katika ”al-Iqtidhwaa´”, uk. 182:
“Ama kuchinja huko – yaani karibu na makaburi – basi ni jambo lililokatazwa kwa ujumla.”
Wanazuoni wetu na wengine wametaja makatazo hayo kwa ajili ya Hadiyth hii.
Amesema Ahmad katika riwaya ya al-Marwaziy: ”Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

Walikuwa wakifisha mfu miongoni mwao wanachinja ngamia juu ya kaburi lake, basi Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akakataza kuhusu hilo.
Alichukia Abu ´Abdillaah kula nyama yake.
Wanazuuoni wetu wamesema:
”Katika maana ya hili ni kile kinachofanywa na wengi wa watu wa zama zetu katika kutoa swadaqah karibu na kaburi kwa mkate au mfano wake.”
an-Nawawiy amesema katika ”al-Majmuu´” (5/320):
“Ama kuchinja huko – kwa maana makaburini – kumekatazwa kabisa. Hilo limetajwa na wenzetu na wengineo kutokana na Hadiyth hii.”
Ahmad amesema katika riwaya ya al-Marwaziy ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Mambo yalikuwa wanapofiliwa na mtu katika wao basi huchinja ngamia kwenye kaburi lake. Ndipo Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) akakataza jambo hilo.”
Abu ́Abdillaah akachukizwa kula nyama yake.
Marafiki zetu wamesema:
”Katika maana ya hili ni kile kinachofanywa na wengi wa watu wa zama zetu katika kutoa swadaqah kwenye kaburi kwa mkate au mfano wake.”

“Ama kuchinja na kuchanja karibu na kaburi ni jambo lenye kusimangwa kutokana na Hadiyth ya Anas hii.”
Ameipokea Abu Daawuud na at-Tirmidhiy na akasema: ”Ni nzuri na Swahiyh.”
Hili ni ikiwa kuchinja huko ni kwa ajili ya Allaah (´Azza wa Jall). Lakini ikiwa ni kwa ajili ya mwenye kaburi – kama wanavyofanya baadhi ya wajinga – basi hiyo ni shirki ya wazi na kula nyama hiyo ni haramu na ufuska. Allaah (´Azza wa Jall):
وَلَا تَأْكُلُوا مِمَّا لَمْ يُذْكَرِ اسْمُ اللَّـهِ عَلَيْهِ وَإِنَّهُ لَفِسْقٌ
“Na wala msile katika ambavyo havikutajiwa Jina la Allaah, kwani hakika huo ni ufasiki.”[1]
Kwa maana hali ya kuwa ni hivyo – kwamba amechinjwa kwa ajili ya asiye Allaah – kwani huu ndio ufuska wenyewe, kama alivyosema Allaah:
أَوْ فِسْقًا أُهِلَّ لِغَيْرِ اللَّـهِ بِهِ
”… au ufasiki, kimechinjwa kwa ajili ya asiye Allaah.”[2]
kama ilivyo katika ”az-Zawaajir” (1/171) ya al-Faqiyh al-Haytamiy. Pia amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Allaah amemlaani… ”
Imekuja katika upokezi mwingine:
”Mlaaniwa yule mwenye kuchinja kwa ajili ya asiyekuwa Allaah.”
Ameipokea Ahmad (na. 2817, 2915, 2917) kwa cheni ya wapokezi nzuri, kutoka kwa Ibn ´Abbaas, na Muslim (6/84) kutoka kwa ´Aliy ambaye amepokea mfano wake.
2 – Kuinua kaburi zaidi ya udongo uliotoka humo.
3 – Kuipaka chokaa au mfano wake.
4 – Kuandika juu yake.
5 – Kujenga juu yake.
6 – Kulikalia.
Zipo Hadiyth kadhaa kuhusu hayo:
1 – Jaabir (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:
“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza kuchokaa kaburi, kuikalia na kujenga juu yake [au kuongeza juu yake], [au kuandika juu yake].”
Ameipokea Muslim (3/62), Abu Daawuud (2/71), an-Nasaa’iy (1/284–286), at-Tirmidhiy (2/155) ambaye ameisahihisha, al-Haakim (1/370), al-Bayhaqiy (4/4) na Ahmad (3/295, 332, 339, 399). Ziada mbili ni za Abu Daawuud na an-Nasaa’iy, na ya kwanza ni ya al-Bayhaqiy. Ya pili ipo kwa at-Tirmidhiy na al-Haakim na akaisahihisha cheni ya wapokezi wake na adh-Dhahabiy akaafikiana naye. al-Mundhiriy (4/341) na wengine wameeleza kuwa ina kasoro ya kukatika baina ya Sulaymaan bin Muusa na Jaabir. Lakini hii ni kwa mujibu wa njia ya Abu Daawuud na wengineo. Vinginevyo ameipokea al-Haakim kupitia njia ya Ibn Jurayj, kutoka kwa Abuz-Zubayr, kutoka kwa Jaabir. Cheni ya wapokezi hii ni kwa sharti za Muslim. Ibn Jurayj ameeleza wazi kusikia kutoka kwa Abuz-Zubayr na huyu kutoka kwa Jaabir. Hivyo imeondoka shaka ya kufanywa kwao hadaa. Kwa upande huu imekuja ya kwanza kwa waliotajwa. an-Nawawiy (5/296) amesema:
“Cheni yake ni Swahiyh.”
Kisha akaijengea hoja ya kwamba inapendekeza kutoongeza kaburi zaidi ya udongo uliotoka humo ambapo akasema: “ash-Shaafi´iy amesema:
”Ikiwa ataongeza si vibaya.”
Marafiki zetu wamesema:
”Maana yake si jambo lenye kuchukiza.”
Hili ni kinyume cha dhahiri ya katazo, kwani msingi wa katazo ni haramu. Hivyo lililo sahihi ni alilosema Ibn Hazm katika ”al-Muhallaa” (5/33):
“Si halali kujenga kaburi, kuchokaa na wala kuongeza juu ya udongo wake chochote – na yote hayo yavunjwe.”
Hii ndio dhahiri ya maneno ya Imaam Ahmad ambapo Abu Daawuud amesema katika ”al-Masaa-il”, uk. 158:
“Nimemsikia Ahmad akisema: ”Kusiongezwe juu ya kaburi udongo usiotoka humo, isipokuwa kama atasawazisha kwa ardhi kiasi ambacho hakitambuliki. Ni kama ametoa ruhusa kwa hali hiyo.”
Lakini ametajwa katika ”al-Inswaaf” (2/548), kutoka kwake ya kwamba ni jambo linachukiza tu. Imaam Muhammad katika ”al-Aathaar”, uk. 45):
“Abu Haniyfah ametukhabarisha, kutoka kwa Hammaad, kutoka kwa Ibraahiym ambaye amesema:
”Ilikuwa ikisemwa: ”Inueni kaburi ili litambulike kuwa ni kaburi na lisikanyagwe.” Muhammad akasema: ”Ndio tunachokifanyia kazi na hatuoni kuwa kuongezwe kile kinachozidi kutoka humo. Tunachukia kuwekwa chokaa, kuwekwa udongo wa mfinyanzi au kufanywa msikiti karibu nalo, alama au kuandika juu yake. Tunachukia kutumia matofali ya kuchomwa kujenga juu yake au kuingiza kaburini. Wala hatuoni ubaya kunyunyizia maji juu yake, ambayo ndio maoni ya Abu Haniyfah.”
Hadiyth inafahamisha kwa maana yake kuwa inajuzu kuliinua kaburi kwa kiasi kinachowezekana kwa udongo uliotoka humo. Hicho huwa takriban shibri mojo, jambo ambalo linaenda sambamba na maandiko yaliyotangulia katika masuala ya 107. Kuhusu kuchokaa maana yake ni kulipaka chokaa. Huenda katazo la kuchokaa ni kwa sababu ni aina ya mapambo, kama walivyosema baadhi ya waliotangulia.
Kujengea juu ya hayo, ni ipi hukumu ya kulipaka udongo wa mfinyanzi kaburi? Wanazuoni wamekhitalifiana katika mitazamo miwili:
1 – Machukizo. Imaam Muhammad amenukuliwa akisema hivyo kama nilivonukuu hapo juu. Machukizo kwake ni kwa maana ya haramu anaposema kwa njia isiyofungamana. Abu Hafsw ambaye ni katika Hanaabilah ameonelea pia kuchukiza, kama ilivyo katika ”al-Inswaaf” (2/549).
2 – Hakuna ubaya kufanya hivo. Ameisimulia Abu Daawuud, uk. 158, kutoka kwa Imaam Ahmad. Ameithibitisha katika ”al-Inswaaf”. Ameisimulia at-Tirmidhiy (2/155), kutoka kwa Imaam ash-Shaafi´iy. an-Nawawiy amesema baada yake:
“Wengi wa wanazuoni wetu hawakulitaja jambo hili. Kwa hiyo sahihi ni kuwa hakuna machukizo yoyote ndani yake, kama alivyosema wazi na hakujapokelewa juu yake makatazo.”
Huenda kilicho sahihi ni kuleta upambanuzi kwa namna ifuatayo: ikiwa nia ya kupaka udongo ni kwa ajili ya kulinda kaburi na kukae juu kiasi kilichoidhinishwa na Shari´ah, kuepuka kusambaratishwa na upepo au mvua, basi ni jambo linaloruhusiwa bila shaka kwa sababu linatimiza kusudio linalokubalika katika Shari´ah. Huenda huu ndio upande wa wale walioona miongoni mwa Hanaabilah kwamba inapendeza. Ikiwa nia ya kupaka ni kwa ajili ya mapambo na mfano wake katika mambo yasiyo na faida yoyote, basi haifai, kwa sababu ni jambo lililozuliwa.
Kuhusu kuandika juu ya kaburi, dhahiri ya Hadiyth ni kwamba ni haramu. Hii ndio dhahiri ya maneno ya Imaam Muhammad. Shaafi´iyyah na Hanaabilah wameelezea wazi ya kwamba inachukiza tu. an-Nawawiy (5/298) amesema:
“Marafiki zetu wamesema kwamba ni mamoja kile kilichoandikwa juu ya kaburi kiko kwenye ubao uliowekwa kichwani, kama ilivyozoeleka kwa baadhi ya watu, au si hivyo, yote hayo ni yenye kuchukiza kutokana na kuene akwa Hadiyth.”
Baadhi ya wanazuoni wamebagua kuandika jina la maiti, si kwa njia ya mapambo, bali kwa kutambulika. Wametumia kipimo juu ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuweka jiwe juu ya kaburi la ´Uthmaan bin Madh´uun, kama ilivyotajwa katika masuala yaliyotangulia, uk. 155. ash-Shawkaaniy amesema:
“Jambo hili ni katika aina ya kutenga kwa kipimo, jambo ambalo limesemwa na kikosi kikubwa cha wanazuoni, si kwamba ni kipimo kinachopinga maandiko, kama alivyosema katika ”Dhaw’-un-Nahaar”. Hata hivyo hoja iko katika kusihi kwa kipimo hiki.”
Ninachoona – na Allaah ndiye mjuzi zaidi – ni kwamba kusema kwamba kipimo hiki ni sahihi kwa ujumla wake ni jambo liko mbali. Sahihi ni kulifunga hilo kwa sharti: ikiwa jiwe haliwezi kufanikisha lengo lililokusudiwa na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) – nalo ni kutambua kaburi hilo – kwa mfano kwa sababu ya wingi wa makaburi au wingi wa mawe ya kutambulisha, basi wakati huo inajuzu kuandika jina kwa kiasi cha kutimiza lengo hilo – na Allaah ndiye mjuzi zaidi. Kuhusu maneno ya al-Haakim baada ya Hadiyth:
“Si jambo lenye kufanyiwa kazi. Kwani wanazuoni wa waislamu, kutoka mashariki hadi magharibi, kumeandikwa juu ya makaburi yao. Nalo ni jambo lililochukuliwa na waliokuja nyuma kutoka kwa waliotangulia.”
adh-Dhahabiy akamraddi kwa kusema:
“Hujasema jambo lenye maana. Wala hatujui Swahabah yeyote aliyefanya hivyo. Ni jambo lililozuliwa na baadhi ya wanafunzi wa Maswahabah na wale waliokuja baada yao baada ya kuwa hawakufikiwa na katazo.”
3 – Abul-Hayyaaj al-Asadiy amesema
“´Aliy bin Abiy Twaalib alinambia: ”Je, nikutume juu ya yale aliyonituma Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)? Kwamba usiachane sanamu lolote… ”
Imekuja katika upokezi mwingine:
”… picha yoyote] [ndani ya nyumba] isipokuwa umeiharibu wala kaburi lililoinuliwa isipokuwa ulisawazishe.”
Ameipokea Muslim (3/61), Abu Daawuud (2/70), an-Nasaa’iy (51/28), at-Tirmidhiy (2/153-154) ambaye ameifanya kuwa nzuri, al-Haakim (1/369), al-Bayhaqiy (4/3), at-Twayaalisiy kwa (na. 155), Ahmad (na. 741, 1064) kwa njia ya Abu Waa-il kutoka kwake na at-Twabaraaniy katika ”al-Mu´jam as-Swaghiyr”, uk. 29 kwa njia ya Abu Ishaaq kutoka kwake.
Ipo pia katika ”Musnad” ya at-Twayaalisiy (na. 96) na Ahmad (na. 657, 658, 683, 689) kuna njia mbili nyingine kutoka kwa ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anh).
ash-Shawkaaniy (Rahimahu Allaah) (4/72) amesema alipokuwa anatoa maelezo ya Hadiyth hii:
”Ndani yake kuna ya kwamba Sunnah ni kuwa kaburi lisiinuliwa juu kwa kiwango kikubwa, bila ya kutofautisha kati ya mwenye ubora na asiyekuwa na ubora. Dhahiri ni kwamba kuinua makaburi zaidi ya kiwango kilichoidhinishwa ni haramu. Hili limetamkwa wazi na wanafunzi wa Ahmad, kikosi cha ash-Shaafi´iy na Maalik.”
Akaendelea kusema:
”Miongoni mwa yale yanayoingia ndani ya katazo la kuinua makaburi ni pamoja na yale makaburi ya wale wanaoitwa ”mawalii wa Allaah”, ambayo yamejengewa majumba na makaburi yenye miundo mizuri. Isitoshe kufanya hivo pia ni sehemu ya kuyafanya makaburi kuwa kama misikiti. Aidha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amemlaani anayefanya hivyo, kama itakavyokuja. Ni madhara mangapi ambayo yamezuka kutokana na kuimarishwa na kupambwa kwa makaburi kiasi cha kulia kwa ajili ya Uislamu? Miongoni mwake ni wajinga kuwa na imani fulani juu ya makaburi haya, kama walivyoamini makafiri juu ya masanamu, jambo hili likakuzwa kiasi cha kudhani kwamba yana uwezo wa kuleta manufaa na kuondoa madhara, wakayaelekea kwa ajili ya kutaka mahitaji yao yatimizwe, wakayaona kuwa ndio hifadhi ya mafanikio yao, wakayaomba yale ambayo waja wanatakiwa waombe kwa Allaah peke Yake, wakafunga safari kuwafuata, wakayapanguza na kuyaomba msaada. Kwa jumla hawakuacha jambo lolote ambalo washirikina walilokuwa wakilitenda kwa masanamu isipokuwa walilitenda. Pamoja na uovu huu mkubwa na kufuru hii mbaya sana, hatuoni mwenye kuyaghadhibikia kwa ajili ya Allaah wala mwenye kuwa na wivu kwa ajili ya dini ya Kiislamu – si mwanachuoni, mwanafunzi, kiongozi, waziri wala mfalme. Zimetufikia khabari zisizo na shaka kuwa wengi wa hawa wanaoshikamana na makaburi, au hata wengi zaidi yao, wanapolazimishwa kuapa kwa Allaah dhidi ya hasimu wao, wanaapa kwa uongo, lakini wakiambiwa: “Apa kwa Shaykh wako au walii wako fulani”, basi wanatetemeka, wanachanganyikiwa, wanakataa na wanakiri haki. Hili ni miongoni mwa dalili zilizo wazi kabisa kuwa ushirikina wao umefikia zaidi ya ushirikina wa wale waliodai kuwa Allaah ni wa pili katika wawili au wa tatu katika watatu. Basi enyi wanazuoni wa dini na enyi wafalme wa Kiislamu! Ni msiba gani mkubwa kwa Uislamu kuliko kufuru? Ni balaa gani juu ya dini hii kubwa kuliko kuabudiwa kwa mwingine asiyekuwa Allaah? Ni msiba gani unaowapata waislamu unaolingana na msiba huu? Ni maovu gani ambayo ni lazima kuyakaripia ikiwa si lazima kukaripia shirki hii?
Ungesikika kama ungemwita aliye hai
lakini hakuna uhai kwa anayeitwa
Na lau ungepuliza moto ungewaka
lakini unavuma kwenye majivu.”
ash-Shawkaaniy (Rahimahu Allaah) ana kijitabu kifupi chenye manufaa katika mlango huu kwa jina ”Sharh-us-Swuduur fiyt-Tahriym Rafiyl-Qubuur” kilichochapishwa katika ”al-Majmuu´ah al-Muniyriyyah” (1/62–76).
4 – Thumaamah bin Shufa´y ameeleza:
”Tulitoka pamoja na Fadhwaalah bin ‘Ubayd kwenda ardhi ya warumi. Alikuwa ni mtumishi wa Mu‘aawiyah kwenye dori.”
Imekuja katika upokezi mwinigine:
”Tulivamia ardhi ya warumi. Katika jeshi hilo alikuwa Fadhwaalah bin ‘Ubayd al-Answariy. Akapigwa binamu yetu Rhodes[3]. Fadhwaalah akamswalia na akasimama juu ya kaburi lake mpaka alipomzika. Alipolinyanyua kaburi lake akasema: ”Mficheni.”
Imekuja katika upokezi mwingine:
”Mpenyeni kidogo juu yake. Hakika Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akituamrisha tusawazishe makaburi.”
Ameipokea Ahmad (6/18) mapokezi yote mawili kwa cheni ya wapokezi nzuri na Ibn Abiy Shaybah (4/135-138) kwa upokezi mwingine. Ameipokea pia Muslim (3/61), Abu Daawuud (2/70), an-Nasaa’iy (1/285) na al-Bayhaqiy (4/2-3) kwa njia nyingine kutoka kwa Thumaamah mfano wake kwa maneno mafupi zaidi. Upokezi wa Ahmad (6/21) unasema:
”Nimesikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema: ”Sawazisheni makaburi yenu na ardhi.”
Katika cheni ya wapokezi wake yumo Ibn Luhay‘ah ambaye ni dhaifu kumbukumbu. Kuhusu Hadiyth maarufu miongoni mwa watu kwa tamko lisemalo:
“Makaburi yaliyo bora zaidi ni yale yaliyochakaa.”
haina msingi wowote katika vitabu vya Sunnah. Kwa udhahiri wake ni dhaifu na yenye kupíngana na Hadiyth zilizo Swahiyh, kwani kaburi halitakiwi kuchakaa kabisa, bali inatakiwa liwe dhahiri limenyanyuliwa kutoka ardhini kwa kiasi cha shibri moja, kama ilivyotajwa awali, ili litambulike na hivyo lihifadhiwe na lisitwezwe, litembelewe na lisisuswe. Jengine ni kwamba dhahiri ya Hadiyth ya Fadhwaalah isemayo:
“Alikuwa akituamrisha tusawazishe makaburi.”
inaonyesha kuwa makaburi yasinyanyuliwe kabisa juu ya ardhi. Hili siyo kusudio, kwani Sunnah ni kuinua kwa shibri moja, kama ilivyoashiriwa awali. Kinachothibitisha hili ni maneno ya Fadhwaalah ndani ya Hadiyth hiyohiyo:
“Mpenyeni… ”
Kwa maana punguzeni udongo juu yake. Kwa maana ya kwamba hakuamrisha kuondoa udongo kabisa juu yake. Hivi ndivyo walivyofasiri wanazuoni. Tazama ”al-Mirqaah” (2/372).
5 – Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Ni bora kwa mmoja wenu kuketi juu ya jiwe lenye moto likachoma nguo zake mpaka limfikie ngozi yake, kuliko kuketi… ”
Imekuja katika upokezi mwingine:
”… kukanyaga] juu ya kaburi.”
Ameipokea Muslim (3/62), Abu Daawuud (2/71), an-Nasaa’iy (1/287), Ibn Maajah (1/484), al-Bayhaqiy (4/79) na Ahmad (2/311, 389, 444). Upokezi mwingine ni miongoni mwa mapokezi yake (2/528).
6 – ´Uqbah bin ´Aamir (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Kunapendeza zaidi kwangu kutembea juu ya jiwe la moto au upanga au nishone kiatu changu kwa miguu yangu[4] kuliko kutembea juu ya kaburi la muislamu. Wala sijali kama nitajisaidia katikati ya kaburi au katikati ya soko.”
Ameipokea Ibn Abiy Shaybah (4/133) na Ibn Maajah (1/474) kwa cheni ya wapokezi Swahiyh, kama alivyosema al-Buuswayriy katika ”az-Zawaa-id” (karatasi 98/1). al-Mundhiriy amesema katika ”at-Targhiyb”:
”Cheni yake ni nzuri.”
7 – Abu Marthad al-Ghanawiy amesema kuwa amemsikia Mtume wa Alllaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:
“Msiswali kuelekea makaburi na wala msiketi juu yake.”
Ameipokea Muslim (3/62) na watunzi wa as-Sunan tatu na wengineo. Kuna nyingine inayoitia nguvu kutoka kwa Hadiyth ya Ibn ‘Abbaas. Ameipokea adh-Dhwiyaa´ al-Maqdisiy katika ”al-Ahaadiyth al-Mukhtaarah”. Nami nimezungumza juu ya cheni yake katika ”Takhriyj Swifati Swalaat-in-Nabiy (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kisha katika ”Tahdhiyr-us-Saajid”, uk. 21.
[1] 06:121
[2] 06:145
[3] Kisiwa kinachojulikana sana katika Bahari ya Mediterania, kusini-magharibi mwa Uturuki.
[4] Kwa maana kwamba hilo ni jambo gumu sana iwapo inawezekana.
- Muhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz wa Bid´ahaa, uk. 258-268
- Imechapishwa: 10/08/2026

Muhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz wa Bid´ahaa, uk. 258-268
Imechapishwa: 10/08/2026
https://firqatunnajia.com/134-mambo-ya-haramu-kuhusiana-na-makaburi/