124 – Wala haijawekwa katika Shari´ah kuweka mihadasi na mfano wake miongoni mwa maua ya harufu nzuri na waridi juu ya makaburi, kwa sababu halikuwa ni katika matendo ya Salaf. Lau ingelikuwa ni kheri wangetutangulia kuyafanya. Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesema:
“Kila Bid´ah ni upotofu, hata kama watu wataiona kuwa ni nzuri.”
Ameipokea Ibn Battwah katika ”al-Ibaanah ´an Usuwl-id-Diyaanah” (2/112/2) na al-Laalakaa’iy katika ”as-Sunnah.”
Haya tuliyoyataja hayapingani na Hadiyth ya Ibn ´Abbaas kuhusu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuweka vipande viwili vya tawi la mtende juu ya makaburi mawili na akasema:
“Huenda wawili hao wakapunguziwa muda wa kuwa havijakauka.”
Kuna maafikiano juu yake. Nimeitaja katika ”Swahiyh Abiy Daawuud” (15).
Hiyo ni maalum kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa dalili ya kwamba haikuwa ni miongoni mwa matendo ya Salaf na kutokana na mambo mengine ambayo itakuja ubainifu wake. al-Khattwaabiy (Rahimahu Allaah) amesema katika ”Ma´aalim-us-Sunan” (1/27) hali ya kuitolea maelezo Hadiyth hiyo:
“Hakika ni katika kutafuta baraka kwa athari ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na du´aa yake ya kuwapunguzia adhabu. Ni kana kwamba ameweka muda wa kubaki kwa unyevunyevu ndani ya makuti hayo kama mpaka wa muda wa suala hilo la kupunguziwa adhabu juu yao. Haina maana kwamba katika kuti mbichi kuna maana fulani isiyokuwamo katika lile lililokauka. Watu wa kawaida katika miji mingi hupanda majani juu ya makaburi ya wafu wao. Naona kuwa wameegemea juu ya hili. Hakuna msingi wa kile wanachokifanya.”
Shaykh Ahmad Shaakir amesema katika maelezo yake juu ya at-Tirmidhiy (1/103) baada ya haya:
“al-Khattwaabiy amesema kweli. Watu wa kawaida wamefanya kupitiliza katika jambo hili lisilo na msingi na wakachupa mipaka juu yake, khaswa katika nchi ya Misri, kwa kuwaiga manaswara. Hali imefikia kwamba wameanza kuweka maua juu ya makaburi na kupeana zawadi ya maua baina yao. Watu huyaweka juu ya makaburi ya jamaa na marafiki zao kama salamu kwao na kama heshima kwa walio hai. Hata ikawa ni desturi karibu rasmi katika muktadha wa heshima za kitaifa ambapo ukawakuta viongozi wa Kiislamu wanaposhuka katika miji ya Ulaya basi huenda kwenye makaburi ya wakuu wao au kwenye kile wanachokiita ”askari asiyejulikana” na kuweka maua juu yake. Baadhi yao huweka maua ya plastiki yasiyo na unyevunyevu kwa kuwaiga wafaransa na kwa kufuata mila za waliokuwa kabla yao. Hakuna yeyote miongoni mwa wanazuoni wanaowakemea watu hao. Bali utawakuta wao wenyewe wakiweka maua hayo kwenye makaburi ya wafu wao. Hakika nimejua kuwa sehemu kubwa ya mali za Waqf zinazojulikana kama ”Waqf za kheri” zimewekewa matumizi ya kununulia majani na waridi vinavyowekwa juu ya makaburi. Haya yote ni Bid´ah na maovu yasiyo na msingi wowote katika dini wala hazina dalili yoyote kutoka katika Qur-aan wala Sunnah. Ni wajibu kwa wanazuoni kuzikaripia na kuzisambaratisha ada hizi kwa kadiri ya uwezo wao.
Kinachotilia nguvu ya kwamba kuweka kuti la mtende juu ya kaburi ni jambo maalum kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kupunguzwa kwa adhabu hakukuwa kwa sababu ya unyevunyevu wa kuti hilo ni mambo yafuatayo:
1 – Hadiyth ya Jaabir (Radhiya Allaahu ´anh) ndefu katika ”as-Swahiyh” ya Muslim (8/231-236) na ndani yake amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Hakika nilipita karibu na makaburi mawili ambayo walikuwa wakiadhibiwa, nikapenda kwa sababu ya maombezi yangu, adhabu ipunguzwe juu yao maadamu matawi hayo mawili bado ni mabichi.”
Hii ni dalili wazi kuwa kuondolewa kwa adhabu kulikuwa kwa sababu ya maombezi yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na du´aa yake, si kwa sababu ya unyevunyevu. Ni mamoja iwe tukio hili la Jaabir ni lilelile na tukio la Ibn ´Abbaas, walivyoyapa nguvu hayo baadhi ya wanazuoni kama al-´Ayniy na wengineo au ni tukio tofauti, kama walivyoyapa nguvu hayo Haafidhw katika ”al-Fath”. Ikiwa uwezekano ni ule wa kwanza basi jambo liko wazi, na ikiwa ni uwezekano wa pili basi fikira sahihi inahitaji sababu katika matukio yote mawili iwe moja kutokana na kufanana kwao. Aidha kwa kuwa kuamini kuwa unyevunyevu ndio sababu ya kupunguzwa kwa adhabu kwa maiti ni jambo lisilojulikana kwa mujibu wa Shari´ah wala akili. Lau jambo lingekuwa hivo, basi watu ambao wangepunguziwa zaidi adhabu wangekuwa ni makafiri wanaozikwa katika makaburi yenye kufanana na bustani kwa wingi wa mimea na miti ambayo daima ni mibichi wakati wa kiangazi na baridi.
Zaidi ya hayo baadhi ya wanazuoni, kama as-Suyuutwiy, wametaja kuwa sababu ya athari ya unyevunyevu katika kupunguza adhabu ni kuwa majani hayo humsabihi Allaah (Ta´ala). Wakasema kwamba unyevunyevu ukikauka basi kunakoma kule kumtaja. Maelezo haya yanakinzana na kuenea kwa maneno Yake (Tabaarak wa Ta´ala):
”wa min shain illa yusabihu….tasbihahum”
2 – Katika Hadiyth yenyewe ya Ibn ´Abbaas kuna kinachoashiria kuwa siri haipo katika unyevunyevu, au kwa uwazi zaidi, unyevunyevu siyo sababu ya kupunguzwa kwa adhabu. Hayo ni maneno yake:
”Kisha akaomba tawi na akalipasua vipande viwili.”
Bi maana kwa urefu. Ni jambo linalojulikana ya kuwa kuipasua ni sababu ya kukauka haraka na hivyo muda wa kupunguzwa kwa adhabu unakuwa mfupi zaidi kuliko kama asingelipasua. Basi lau hiyo ndiyo ingelikuwa sababu, basi angeacha ikiwa nzima, au angeliweka kila kuti moja au nusu yake juu ya kila kaburi angalau. Kwa kuwa hakufanya hivyo, basi ni dalili kuwa unyevunyevu siyo sababu, bali ni ishara ya muda wa kupunguzwa kwa adhabu ambao Allaah ameruhusu kwa kuitikia maombezi ya Mtume wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kama ilivyotajwa wazi katika Hadiyth ya Jaabir. Kwa hivyo Hadiyth hizi mbili zinakubaliana katika kubainisha sababu, hata kama kuna uwezekano wa kutofautiana katika matukio na kuzidi kwa idadi yake. Basi tafakari hili, kwani ni jambo lililotokea moyoni mwangu na wala sijaona mwenye kulitaja wazi au kulieleza miongoni mwa wanazuoni. Ikiwa ni sahihi basi ni kutoka kwa Allaah (Ta´ala), na ikiwa ni kosa, basi ni kutoka kwangu na namuomba msamaha kwa kila jambo lisilomridhisha.
3 – Lau unyevunyevu ndio ulilengwa kimsingi, basi hilo lingefahamika na Salaf na wangelitenda kwa mujibu wake. Hivyo wangeweka vikonyo na mfano wake juu ya makaburi wakati wanayatembelea. Lau wangelifanya hilo, basi lingejulikana kuhusu wao, kisha waaminifu wangetufikishia kwa sababu hilo ni miongoni mwa mambo yanayovutia macho na yanayochochea hamu ya kuhadithia. Basi kwa kuwa halikupokelewa basi ikajulisha ya kuwa halikutokea na kwamba kujikurubisha kwa Allaah kwa hilo ni Bid´ah. Hivyo makusudio yamethibiti. Ikiwa hili limebainika, basi huwa rahisi wakati huo kuelewa ubatilifu wa kipimo dhaifu ambacho kimesimuliwa na as-Suyuutwiy katika ”Sharh-us-Swuduur” kutoka kwa ambaye hakumtaja jina:
”Ikiwa wamepunguziwa kwa tasbihi ya kijiti cha mtende, basi vipi kuhusu usomaji wa muumini wa Qur-aan?” Akasema: ”Hadiyth hii ndio msingi wa kupanda miti juu ya makaburi.”
Anaambiwa:
”Simamisha kiti ndio utie nakshi.”
”Je, kivuli kitakuwa sawa ikiwa chenyewe kimepinda?”
Kipimo hiki kingekuwa sahihi, basi Salaf wangekimbilia kukifanya kwa kuwa wao ni wenye kupupia zaidi kheri kuliko sisi. Basi yaliyotangulia yanaonyesha kuwa kuweka kijiti cha mtende juu ya kaburi ni jambo maalum kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kwamba siri ya kupunguzwa adhabu kwa wale wawili haikuwa katika unyevunyevu wa kijiti, bali ilikuwa katika uombezi wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na du´aa yake kwao, jambo ambalo haliwezi kutokea tena baada ya yeye (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwenda kwa Mola Wake na wala halipo kwa yeyote baada yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kwa sababu kufunuliwa khabari kuhusu adhabu ya kaburini ni miongoni mwa mambo maalum kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Aidha ni miongoni mwa mambo ya ghaibu ambayo hapewi yeyote isipokuwa tu Mtume aliyechaguliwa, kama ilivyotajwa ndani ya Qur-aan:
عَالِمُ الْغَيْبِ فَلَا يُظْهِرُ عَلَىٰ غَيْبِهِ أَحَدًا إِلَّا مَنِ ارْتَضَىٰ مِن رَّسُولٍ
”Mjuzi wa mambo yaliyofichikana na wala hamdhihirishii yeyote ghaibu Yake, isipokuwa yule aliyemridhia ambaye ni Mtume.”[1]
Fahamu ya kuwa halipingani na yale tuliyobainisha yale aliyoyanukuu as-Suyuutwiy katika ”Sharh-us-Swuduur” (131):
”Ibn ´Asaakir amepokea kwa njia ya Hammaad bin Salamah, kutoka kwa Qataadah ya kwamba Abu Barzah al-Aslamiy (Radhiya Allaahu ´anh) alikuwa akihadithia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipita kwenye kaburi na mwenye kaburi hilo alikuwa akiadhibiwa. Basi akachukua kijiti cha mtende akakipandikiza juu ya kaburi na akasema: ”Huenda adhabu ikapunguzwa juu yake muda wa kuwa kitabaki na unyevunyevu.” Abu Barzah alikuwa akiusia: ”Nikifa wekeni pamoja nami makaburini vijiti viwili vya mtende.” Akasema: ”Akafariki akiwa porini kati ya Kirmaan na Quumis, wakasema: ”Alikuwa akituusia kuweka makaburini mwake vijiti viwili vya mtende, lakini hapa hatuvipati. Walipokuwa katika hali hiyo, ghafla wakaja watu kutoka Sijistaan ambao walikuwa na majani ya mitende. Wakachukua vijiti viwili na wakavipandikiza kwenye kaburi lake.”
Ibn Sa´d amepokea kutoka kwa Muwarraq ambaye amesema:
”Buraydah aliacha wasia kwamba vijiti viwili vya mtende viwekwe katika kaburi lake.”
Njia ya kutokuwapo upinzani ni kwamba hakuna katika masimulizi haya mawili – hata kama tutakubali kuwa yote mawili yamesihi – usuniwaji wa kuweka vijiti vya mtende wakati wa kuzuru makaburi, jambo ambalo tumelihukumu kuwa ni Bid´ah kwa sababu Salaf hawakulitenda. Kubwa liliopo katika matukio hayo mawili ni kuweka vijiti viwili pamoja na maiti ndani ya kaburi, na hili ni jambo tofauti, hata kama linafanana na lile la awali kwa kutokuwepo usuniwaji wake. Hadiyth iliyopokelewa na Abu Barzah kama ilivyo kwa Maswahabah wengine haifahamishi hivo, khaswa ukizingatia kwamba Hadiyth inasema aliweka kijiti kimoja tu, naye aliusia kuweka viwili kaburini mwake. Zaidi ya hayo masimulizi hayo cheni yake ya wapokezi haikusihi. al-Khatwiyb amepokea katika ”Taariykh Baghdaad” (1/182-183), na kwa njia yake Ibn ´Asaakir amepokea katika ”Taariykh Dimashq” mwishoni mwa wasifu wa Nadhwah bin ´Ubayd bin Abiy Barzah al-Aslamiy, kutoka kwa ash-Shaah bin ´Ammaar ambaye amesema: Abu Swaalih Sulaymaan bin Swaalih al-Laythiy ametuhadithia kwa kusema: an-Nadhwr bin al-Mundhir bin Tha´labah al-´Abdiy ametuhadithia, kutoka kwa Hammaad bin Salamah kwa hivyo.”
Hii ni cheni ya wapokezi ambayo ni dhaifu ambayo ina kasoro mbili:
1 – Kutokujulikana kwa ash-Shaah na an-Nadhwr, kwa kuwa sikuona wasifu.
2 – Qataadah hakutaja wazi ni namna gani amepokea, kwani hakutaja kuwa amepokea kutoka kwa Abu Barzah. Isitoshe ametajwa kuwa ni mwenye kufanya hadaa. Kwa hivyo kunakhofiwa kuwa amefanya hadaa katika mfano wa cheni yake kama hii.
Ama wasia wa Buraydah ni jambo limethibiti kutoka kwake. Ibn Sa´d amesema katika ”at-Twabaqaat” (7/1-4):
”´Affaan bin Muslim ametukhabarisha: Hammaad bin Salamah ametuhadithia: ´Aaswim al-Ahwal ametuhadithia: Muwarraq amesema: ”Buraydah al-Aslamiy aliusia kuwekwe katika kaburi lake vijiti viwili vya mtende. Basi alipofariki karibu na Khuraasaan na havikupatikana isipokuwa ndani ya gunia la punda.”
Cheni hii ya wapokezi ni Swahiyh ya wapokezi na ameipokea al-Bukhaariy (3/173) ikiwa ni cheni ya wapokezi pungufu kwa namna ya uhakika.
Haafidhw amesema katika maelezo yake:
”Buraydah aliichukulia Hadiyth kwa kuenea kwake na hakuona kuwa ni maalum kwa wale wawili.”
Ibn Rushayd amesema:
”Inaonekana kutoka kwa namna alivyofanya al-Bukhaariy kuwa jambo hilo ni maalum kwa mabwana hao wawili. Kwa ajili hiyo ndio maana akafuatisha kwa maneno ya Ibn ´Umar: ”Hakika kinachomfunika ni matendo yake.”
Hapana shaka ya kuwa alivyoona al-Bukhaariy ndiyo sahihi kwa mujibu wa yaliyotangulia kubainishwa. Maoni ya Buraydah si hoja ndani yake, kwa sababu ni maoni tu. Isitoshe Hadiyth haijulishi hivyo, hata kama ingelikuwa ni yenye kuenea, kwani Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakuweka kijiti juu ya kaburi, bali mambo yalivyo ni kwamba:
”Mwongozo bora ni mwongozo wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).”
[1] 72:26
- Muhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz wa Bid´ahaa, uk. 253-258
- Imechapishwa: 10/08/2026

Muhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz wa Bid´ahaa, uk. 253-258
Imechapishwa: 10/08/2026
https://firqatunnajia.com/133-makatazo-ya-kuweka-vijiti-na-maua-juu-ya-makaburi/