al-Qummiy amesema alipokuwa akifasiri maneno Yake (Ta´ala):
وَمَنْ خَفَّتْ مَوَازِينُهُ فَأُولَـٰئِكَ الَّذِينَ خَسِرُوا أَنفُسَهُم بِمَا كَانُوا بِآيَاتِنَا يَظْلِمُونَ
“Na ambao mizani yao itakuwa miepesi, basi hao ni wale waliokhasirika nafsi zao kwa yale waliyokuwa wakizifanyia dhuluma Aayah Zetu.”[1]
“Bi maana wanawakanusha maimamu.”[2]
Haya ni makengeusho ya Baatwiniyyah. Allaah hakumuamrisha yeyote kuwaamini maimamu. Yule asiyewajua asiwaulizie. Yule mwenye kupinga uongozi wao ambao umezuliwa na Raafidhwah Baatwiniyyah huyo ndiye kapatia. Yule mwenye kuchukulia wepesi haki ya nduguzo anapata dhambi.
Kuhusu Aayah ambazo Allaah ametishia kwazo, inahusiana na Aayah za kilimwengu, na khaswa khaswa miujiza inayofahamisha ukweli wa Mitume wake, na Aayah Zake za Kishari´ah ambazo ameziteremsha katika Kitabu Chake kuwateremshia Mitume Wake. Aayah hizo zinakokoteza katika Tawhiyd, kupiga vita shirki, kutoa khabari kuhusu Pepo, Pepo, hesabu, malipo na mengineyo ambayo yamefikishwa na Mitume watukufu (Swalla Allaahu ´alayhim wa sallam).
[1] 07:09
[2] Tafsiyr al-Qummiy (1/224).
- Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 195
- Imechapishwa: 14/07/2018
al-Qummiy amesema alipokuwa akifasiri maneno Yake (Ta´ala):
وَمَنْ خَفَّتْ مَوَازِينُهُ فَأُولَـٰئِكَ الَّذِينَ خَسِرُوا أَنفُسَهُم بِمَا كَانُوا بِآيَاتِنَا يَظْلِمُونَ
“Na ambao mizani yao itakuwa miepesi, basi hao ni wale waliokhasirika nafsi zao kwa yale waliyokuwa wakizifanyia dhuluma Aayah Zetu.”[1]
“Bi maana wanawakanusha maimamu.”[2]
Haya ni makengeusho ya Baatwiniyyah. Allaah hakumuamrisha yeyote kuwaamini maimamu. Yule asiyewajua asiwaulizie. Yule mwenye kupinga uongozi wao ambao umezuliwa na Raafidhwah Baatwiniyyah huyo ndiye kapatia. Yule mwenye kuchukulia wepesi haki ya nduguzo anapata dhambi.
Kuhusu Aayah ambazo Allaah ametishia kwazo, inahusiana na Aayah za kilimwengu, na khaswa khaswa miujiza inayofahamisha ukweli wa Mitume wake, na Aayah Zake za Kishari´ah ambazo ameziteremsha katika Kitabu Chake kuwateremshia Mitume Wake. Aayah hizo zinakokoteza katika Tawhiyd, kupiga vita shirki, kutoa khabari kuhusu Pepo, Pepo, hesabu, malipo na mengineyo ambayo yamefikishwa na Mitume watukufu (Swalla Allaahu ´alayhim wa sallam).
[1] 07:09
[2] Tafsiyr al-Qummiy (1/224).
Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 195
Imechapishwa: 14/07/2018
https://firqatunnajia.com/135-al-qummiy-upotoshaji-wake-wa-kwanza-wa-al-araaf/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)