Jengine ni kwamba khofu haitakiwi kuambatana na kukata tama. Khofu ikiambatana na kukata tamaa na rehema za Allaah inakuwa ukafiri:
إِنَّهُ لَا يَيْأَسُ مِن رَّوْحِ اللَّـهِ إِلَّا الْقَوْمُ الْكَافِرُونَ
“Hakika hawakati tamaa na faraja ya Allaah isipokuwa watu makafiri.”[1]
Ibraahiym (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
وَمَن يَقْنَطُ مِن رَّحْمَةِ رَبِّهِ إِلَّا الضَّالُّونَ
“Na nani anayekata tamaa na rehema za Mola wake isipokuwa waliopotea.”[2]
Vivyo hivyo kutaraji hakutakiwi kumfanya mtu kujiaminisha na vitimbi vya Allaah na kumfanya akawa hana khofu. Hiyo ndio ´Aqiydah ya Murji-ah – pia ni ´Aqiydah potofu:
أَفَأَمِنُوا مَكْرَ اللَّـهِ ۚ فَلَا يَأْمَنُ مَكْرَ اللَّـهِ إِلَّا الْقَوْمُ الْخَاسِرُونَ
“Je, wameaminisha nja za Allaah? Basi hawaaminishi njama za Allaah isipokuwa watu wenye kukhasirika.”[3]
Kuwa na matarajio peke yake ni ukafiri, na khofu pasi na matarajio pia ni ukafiri. Kwa ajili hiyo mtunzi wa kitabu amesema:
”Kujiaminisha na kukata tamaa yote yanamtoa mtu nje ya Uislamu.”
Ndio maana Salaf wamesema kuwa mja anatakiwa kuwa kati ya khofu na matarajio. Kwa msemo mwingine awe kama mbawa za ndege, mbawa za ndege hulingana. Mbawa moja ikiharibika, basi ndege anaanguka. Hali kadhalika mja anatakiwa kuwa kama mbawa mbili za ndege.
[1]12:87
[2]15:56
[3]7:99
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 143
- Imechapishwa: 18/11/2024
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)