132. Aina mbalimbali za kheri na adabu kwa jumla

  Download

267- “Kunapoingia giza la usiku – au mkaingiliwa na jioni – basi wazuieni watoto wenu kutoka toka nje. Kwani kipindi hicho mashaytwaan wanatawanyika. Ukishapita wakati waacheni.  Na pia fungeni milango yenu  na mlitaje jina la Allaah, kwani hakika shaytwaan hafungui mlango uliofungwa. Pia fungeni viriba vyenu vya maji, mlitaje jina Allaah, funikeni vyombo vyenu na mlitaje jina la Allaah ingawa ni kwa kuweka kitu juu yake. Pia zimeni taa zenu.”[1]

[1] al-Bukhaariy pamoja na al-Fath (10/88) na Muslim (3/1595).

  • Mhusika: Shaykh Sa´iyd bin ´Aliy bin Wahf al-Qahtwaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Huswn-ul-Muslim
  • Imechapishwa: 09/05/2020