Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:
106 –Tunataraji wafanyao wema miongoni mwa waumini atawasamehe na kuwaingiza Peponi kwa rehema Zake. Hatujiaminishi nao na wala hatuwashuhudii kuingia Peponi.
MAELEZO
Haya yanahusu kumshuhudia mtu binafsi kama ataingia Peponi au kama ataingia Motoni. Hatufanyi hivo isipokuwa kwa dalili. Wakati Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anaposema kuwa mtu fulani ataingia Peponi, basi nasi tunasema vivyo hivyo, na wakati Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anaposema kuwa mtu fulani ataingia Motoni, basi tunasema vivyo hivyo. Haya ni kuhusiana na mtu mmoja mmoja kwa dhati zao. Lakini inapokuja kwa mtazamo wa kijumla tunaamini kuwa makafiri wataingia Motoni na kwamba waumini wataingia Peponi. Hata hivyo inapohusu mtu mmoja mmoja kwa dhati zao hatuwezi kufanya hivo pasi na dalili. Lakini tunataraji mema kwa mtenda mema na tunachelea juu ya mtenda dhambi. Hii ndio ´Aqiydah ya waislamu.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 140-141
- Imechapishwa: 17/11/2024
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)