Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

105 – Hatusemi kuwa dhambi haiathiri imani kwa yule mwenye kuitenda.

MAELEZO

Kama wanavosema Murji-ah. Wanasema kuwa midhali mtu anasadikisha kwa moyo wake basi ni muumini mwenye imani kamilifu. Wanachukulia wepesi suala la matendo. Wao wanaona inatosha mtu kuwa muumini maadamu anaamini kwa moyo wake ijapo haswali, hafungi, hahiji, hatoi zakaah na wala hafanyi kitu katika matendo mema. Huu ni upotofu mkubwa kabisa.

Dhambi zinadhuru kwa hali zote. Baadhi ya dhambi zinaiondosha imani kabisa. Dhambi zingine haziiondoshi imani yote, bali zinaipunguza. Katika hali hii wenye nayo wanakuwa khatarini kuadhibiwa.

  • Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 140
  • Imechapishwa: 17/11/2024