al-Qummiy amesema:
“Kisha Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) akasema kumwambia Mtume wake Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
وَإِن تُطِعْ أَكْثَرَ مَن فِي الْأَرْضِ يُضِلُّوكَ عَن سَبِيلِ اللَّـهِ
“Ukiwatii wengi walioko ulimwenguni, basi watakupoteza na njia ya Allaah.”
“Bi maana watakufanya kudangana kutokamana na maimamu. Wao si vyengine ni wenye kutofautiana:
إِن يَتَّبِعُونَ إِلَّا الظَّنَّ وَإِنْ هُمْ إِلَّا يَخْرُصُونَ
“Hakuna jengine wanachofuata isipokuwa dhana na hawakuwa ila wenye kubuni uongo.”[1]
Wanazungumza pasi na elimu. Wanabahatisha na kupekua.”[2]
Njia ya Allaah ni dini Yake ambayo amewawekea Shari´ah waja Wake (kama mfano wa Tawhiyd na Shari´ah nyenginezo).
Halafu mtu anaweza kujiuliza watu wengi ulimwenguni walikuwa tayari wameshatofautiana juu ya imamu tokea hapo Makkah. Imamu tayari alikuwa ni gumzo katika Qur-aan tokea zama hizo? Watu tayari walikuwa katika mivutano kuhusu uongozi katika wakati huo jambo ambalo lilimfanya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kudangana juu ya imamu huyu? Allaah azifanye kuwa mbaya nyuso za waongo na wapumbavu!
Kitu kingine ambacho tunapata kufaidika kutokana na Aayah ni kwamba haki haikufungamana na wafuasi wengi. Watu wengi wanaweza kuwa katika upotevu na batili na haki ikawa na wachache. Aayah nyingi za Qur-aan zimethibitisha namna hiyo ili mizani ya muumini iwe hoja na dalili, na si wingi. Hii ni doja yenye kuangamiza dhidi ya wale wenye kuzipa nguvu sauti nyingi pasi na kujali ni wapi zimetoka.
[1] 06:116
[2] Tafsiyr al-Qummiy (1/215).
- Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 189
- Imechapishwa: 20/06/2018
al-Qummiy amesema:
“Kisha Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) akasema kumwambia Mtume wake Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
وَإِن تُطِعْ أَكْثَرَ مَن فِي الْأَرْضِ يُضِلُّوكَ عَن سَبِيلِ اللَّـهِ
“Ukiwatii wengi walioko ulimwenguni, basi watakupoteza na njia ya Allaah.”
“Bi maana watakufanya kudangana kutokamana na maimamu. Wao si vyengine ni wenye kutofautiana:
إِن يَتَّبِعُونَ إِلَّا الظَّنَّ وَإِنْ هُمْ إِلَّا يَخْرُصُونَ
“Hakuna jengine wanachofuata isipokuwa dhana na hawakuwa ila wenye kubuni uongo.”[1]
Wanazungumza pasi na elimu. Wanabahatisha na kupekua.”[2]
Njia ya Allaah ni dini Yake ambayo amewawekea Shari´ah waja Wake (kama mfano wa Tawhiyd na Shari´ah nyenginezo).
Halafu mtu anaweza kujiuliza watu wengi ulimwenguni walikuwa tayari wameshatofautiana juu ya imamu tokea hapo Makkah. Imamu tayari alikuwa ni gumzo katika Qur-aan tokea zama hizo? Watu tayari walikuwa katika mivutano kuhusu uongozi katika wakati huo jambo ambalo lilimfanya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kudangana juu ya imamu huyu? Allaah azifanye kuwa mbaya nyuso za waongo na wapumbavu!
Kitu kingine ambacho tunapata kufaidika kutokana na Aayah ni kwamba haki haikufungamana na wafuasi wengi. Watu wengi wanaweza kuwa katika upotevu na batili na haki ikawa na wachache. Aayah nyingi za Qur-aan zimethibitisha namna hiyo ili mizani ya muumini iwe hoja na dalili, na si wingi. Hii ni doja yenye kuangamiza dhidi ya wale wenye kuzipa nguvu sauti nyingi pasi na kujali ni wapi zimetoka.
[1] 06:116
[2] Tafsiyr al-Qummiy (1/215).
Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 189
Imechapishwa: 20/06/2018
https://firqatunnajia.com/130-al-qummiy-upotoshaji-wake-wa-kumi-wa-al-anaam/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)