13- Wanawatisha na kuwashtua pasi na kuwa na huruma wale wanaowakosoa au kutahadharisha mfumo wao. Mmoja katika viongozi wao wadogo aliniandikia barua mimi na Shaykh Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy (Rahimahu Allaah), ikiwa imesheheni matusi, maapizo, tuhuma za dhambi na lawama. Linaonyesha chuki yake dhidi ya wale wenye kukosoa mfumo wa al-Ikhwaan unaotembea kwenye nyama na damu yake na unamiliki moyo na ulimi wake.
Pamoja na udogo wa kijitabu nilikipa jina “an-Naqd war-Radd ´alaal-Aqwaal al-Muftaraah”. Niliweka nukta zisizopungua chini ya kumi kwenye kitabu changu “al-Ajwibah as-Sadiydah”[1]. Hili kwa sababu wasomaji wote wajue ni chuki gani al-Ikwaan al-Muslimuun wote walionayo dhidi ya wanafunzi wa Salafiyyuun pasi na kujali uhakika wa mambo elimu ya Salafiyyuun, Da´wah, ukweli na unyenyekevu walio nao. Hayako mbali na yale aliyosema Jaasim al-Muhalhal, mmoja katika viongozi wa al-Ikhwaan al-Muslimuun:
“Da´wah ya al-Ikhwaan inamkataa ambaye yataki kuwa katika mikakati na nidhamu zao hata kama atakuwa ni mlinganizi aliye na uelewa mzuri wa Uislamu na ´Aqiydah, mwenye kusoma sana, aliye na hamasa nyingi na unyenyekevu zaidi katika swalah.”[2][3]
[1] 3/307-308, chapa ya pili.
[2] Lid-Du´aat faqat, uk. 122.
[3] Imaam Swaalih al-Fawzaan amesema:
“Kijitabu hichi kilichoko mbele yetu kimeandikwa na ndugu yetu Shaykh Zayd bin Muhammad bin Haadiy al-Madkhaliy. Kinatahadharisha mifumo hii, kinabainisha athari zake mbaya na kinahimiza kushikamana barabara na mfumo wa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Allaah amjaze kheri na anufaishe kwa nasaha na maelekezo yake.” (Asbaab Istiqaamat-ish-Shabaab wa Bawaa´ith Inhiraafihim, uk. 7)
- Muhusika: ´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Asbaab Istiqaamat-ish-Shabaab wa Bawaa´ith Inhiraafihim, uk. 20
- Imechapishwa: 25/03/2017
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)