Swali 13: Wako wanaosema kuwa ikiwa hakukuadhiniwa mwanzoni mwa wakati basi hakuna haja ya kuadhini. Kwa sababu adhaana ni kwa ajili ya kutangaza kuingia wakati wa swalah. Ni yepi maoni ya muheshimiwa juu ya hayo? Je, adhaana imesuniwa kwa anayeswali peke yake shambani[1]?
Jibu: Ikiwa muadhini hakuadhini mwanzoni mwa wakati basi haikusuniwa kwake kuadhini baada ya hapo. Maeneo hayo pakiweko waadhini wengine basi yamekwishafikiwa malengo. Ikiwa uchelewaji ni kidogo basi hapana vibaya kwa yeye kuadhini. Lakini ikiwa katika nchi hakuna waadhini wengine isipokuwa yeye tu, basi atalazimika kuadhini ijapo atachelewa kidogo. Kwa sababu katika hali hii adhaana ni faradhi kwa baadhi ya watu na hakuna wengine wawezao kufanya hivo. Hivyo kutamuwajibikia kwa sababu yeye ndiye mwenye jukumu ya jambo hilo. Sababu nyingine mara nyingi watu wanamsubiria yeye. Kuhusu msafiri imesuniwa kwake adhaana hata akiwa peke yake. Imethibiti katika “as-Swahiyh” ya kwamba Abu Sa´iyd (Radhiya Allaahu ´anh) alisema kumwambia bwana mmoja:
“Ukiwa kati ya mifugo wako au shambani mwako basi ipaze sauti yako kwa kuadhini. Hakika mimi nimemsikia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:
“Hakuna kinachosikia sauti ya muadhini – iwe mti, jiwe wala chochote chengine – isipokuwa kitamtolea ushuhuda siku ya Qiyaamah.”
Pia kutokana na ujumla wa Hadiyth nyenginezo juu ya uwekwaji Shari´ah wa adhaana na faida zake.
[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (10/349-350).
- Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Ahkaam-ul-Musaafir, uk. 29-30
- Imechapishwa: 27/02/2022
Swali 13: Wako wanaosema kuwa ikiwa hakukuadhiniwa mwanzoni mwa wakati basi hakuna haja ya kuadhini. Kwa sababu adhaana ni kwa ajili ya kutangaza kuingia wakati wa swalah. Ni yepi maoni ya muheshimiwa juu ya hayo? Je, adhaana imesuniwa kwa anayeswali peke yake shambani[1]?
Jibu: Ikiwa muadhini hakuadhini mwanzoni mwa wakati basi haikusuniwa kwake kuadhini baada ya hapo. Maeneo hayo pakiweko waadhini wengine basi yamekwishafikiwa malengo. Ikiwa uchelewaji ni kidogo basi hapana vibaya kwa yeye kuadhini. Lakini ikiwa katika nchi hakuna waadhini wengine isipokuwa yeye tu, basi atalazimika kuadhini ijapo atachelewa kidogo. Kwa sababu katika hali hii adhaana ni faradhi kwa baadhi ya watu na hakuna wengine wawezao kufanya hivo. Hivyo kutamuwajibikia kwa sababu yeye ndiye mwenye jukumu ya jambo hilo. Sababu nyingine mara nyingi watu wanamsubiria yeye. Kuhusu msafiri imesuniwa kwake adhaana hata akiwa peke yake. Imethibiti katika “as-Swahiyh” ya kwamba Abu Sa´iyd (Radhiya Allaahu ´anh) alisema kumwambia bwana mmoja:
“Ukiwa kati ya mifugo wako au shambani mwako basi ipaze sauti yako kwa kuadhini. Hakika mimi nimemsikia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:
“Hakuna kinachosikia sauti ya muadhini – iwe mti, jiwe wala chochote chengine – isipokuwa kitamtolea ushuhuda siku ya Qiyaamah.”
Pia kutokana na ujumla wa Hadiyth nyenginezo juu ya uwekwaji Shari´ah wa adhaana na faida zake.
[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (10/349-350).
Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Ahkaam-ul-Musaafir, uk. 29-30
Imechapishwa: 27/02/2022
https://firqatunnajia.com/13-pindi-muadhini-anapochelewa-kutoa-adhaana-mwanzoni-mwa-wakati/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)