13. Nadharia mbili potevu juu ya Qadar

Makundi mawili yamepotea juu ya Qadar:

1- Kundi linalopinga. Linaamini Qadar na kudai kwamba mja mwenyewe ndiye anayeumba matendo Yake.

2- Kundi linalothibitisha. Wanaamini hali ya kupindukia na wanadai kwamba mja ametenzwa nguvu juu ya matendo yake.

Fikira zote mbili zimezuliwa na zimepindukia. Haki ilio kati na kati ni ´Aqiydah ya kundi lililookoka. Linaamini Qadar na kwamba mja ni mwenye kutenda kwa kutaka kwake mwenyewe. Kwani Allaah (Subhanaahu wa Ta´ala) ndiye kamthibitishia hilo na akasema:

لِمَن شَاءَ مِنكُمْ أَن يَسْتَقِيمَ وَمَا تَشَاءُونَ إِلَّا أَن يَشَاءَ اللَّـهُ رَبُّ الْعَالَمِينَ

“Kwa yule atakaye miongoni mwenu anyooke – na hamtotaka isipokuwa atake Allaah Mola, wa walimwengu.”[1]

Lakini hata hivyo matakwa haya ya khiyari hayatoki nje ya yale ambayo Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amekadiria. Miongoni mwa yale yanayofahamisha juu ya hilo ni maneno ya Allaah (´Azza wa Jall):

فَأَلْهَمَهَا فُجُورَهَا وَتَقْوَاهَا قَدْ أَفْلَحَ مَن زَكَّاهَا

“… Kisha akaitambulisha uovu wake na uchaji wkae. Hakika amefaulu yule aliyeitakasa.”[2]

Hivyo tunapata kujua kwamba mapote haya mawili yaliyopindukia yamepotea. Kundi la kwanza linaitwa “Qadariyyah” na kundi la pili linaitwa “Jabriyyah”.

[1] 81:28-29

[2] 91:8-9

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Itmaam-ul-Minnah, uk. 91
  • Imechapishwa: 08/04/2019