Mbora wa Ummah huu baada ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni Abu Bakr, kisha ´Umar, halafu ´Uthmaan. Kuna jopo la wanazuoni wa Ahl-us-Sunnah ambao wanaona kuwa ´Aliy ndiye mwenye kufata baada ya ´Uthmaan na wengine wakasimama kwa ´Uthmaan. Hawa ndio makhaliyfah waongofu na wenye kuongoza.

Baada ya hawa wanne watu bora ni Maswahabah wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) waliosalia. Haijuzu kwa yeyote kutaja chochote katika mabaya yao. Haifai kwa yeyote kumtukana mmoja katika wao kwa kasoro, upungufu wala dharau. Ambaye atafanya hivo basi ni lazima kwa mtawala kumtia adabu na kumuadhibu. Asimuonee huruma. Bali anatakiwa kumuadhibu kisha amtake kutubia. Akitubia, basi tawbah yake itakubaliwa, na asipotubia, atamuadhibu kwa mara nyingine. Kisha atamfunga mpaka pale atakapotubia na kujirejea. Hii ndio ´Aqiydah juu ya Maswahabah wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

  • Mhusika: Imaam Harb bin Ismaa´iyl al-Kirmaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-us-Sunnah, uk. 70-71
  • Imechapishwa: 30/05/2022